Kylie Jenner katika tuhuma za kufoji vipodozi

0
1308

LOS ANGELES, MAREKANI

MWANAMITINDO wa Marekani, Kylie Jenner, anatuhumiwa na kampuni ya vipodozi ya Sheree Cosmetic kwa kulitumia kimakosa jina la ‘Born to Sparkle’, katika vipodozi vyake.

Kylie anamiliki kampuni ya Kylie Cosmetics ambayo hivi karibuni ilizindua vipozi vilivyokuwa na jina la ‘Born to Sparkle’ linalomaanisha mrembo wa maisha, lakini kampuni ya Sheree Cosmetic imedai kulimiliki jina hilo muda mrefu.

Taarifa ya Sheree Cosmetic ilitolewa juzi ikiwa siku chache tangu Kylie azindue bidhaa zake wakati wa shehere ya kuzaliwa kwake.

Kampuni ya Sheree Cosmetic inamiliki jina hilo tangu Agosti 30 mwaka huu lakini Kylie alishindwa kutolea ufafanuzi kuhusu ukweli wa jambo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here