24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

KYLIE JENNER ASHAMBULIWA KWA KUMTOBOA MWANAYE SIKIO

NEW YORK, MAREKANI

KYLIE Jenner, mwanamitindo ambaye wiki iliyopita alitajwa na Jarida la Forbes kuwa staa bilionea mwenye umri mdogo, ameshambuliwa na mashabiki kutokana na kitendo chake cha kumtoboa sikio mtoto wake.

Ni miezi mitano sasa tangu mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20 afanikiwe kupata mtoto wa kwanza ambaye anajulikana kwa jina la Stormi.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Kylie aliposti picha ya mtoto huyo ikimuonesha kuwa masikio yake yametobolewa na amevishwa hereni za rangi ya dhahabu.

Kitendo cha mtoto huyo kutobolewa sikio kumemfanya Kylie ashambuliwe na mashabiki kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakidai ni maamuzi yake kumfanya mtoto apendeze tangu akiwa mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles