MPENZI wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Tyga, Kylie Jenner, ameamua kujifunza kupika kwa ajili ya kuwa mke bora kwa msanii huyo.
Mrembo huyo ameamua kutumia muda wake kutembelea familia ya Kardashian kwa ajili ya kujifunza kupika chakula.
“Ni jambo zuri kwa mwanamke kujua kupika na wengi hawajui kupika, lakini kwa upande wangu naweza kupika kutokana na elimu ninayoipata na familia yangu.
“Wanaume wengi wanapenda mke ajue kupika, hivyo ni lazima nijue ili nisije nikakimbiwa na mpenzi wangu,” aliandika Kylie kwenye akaunti yake ya Instagram.