30.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Kwanini watu hupenda kusengenya?

INASEMEKANA, maarifa ni nguvu lakini iwe kweli au hapana watu wengi hupenda kusambaza taarifa potofu au zenye kutisha dhidi ya watu wengine  ambazo kimsingi ndizo huitwa masengenyo. Kwa vyovyote vile masengenyo  hutumiwa  na watu kuumiza wengine ili wao waendelee kujihisi wako vizuri au wana nguvu zaidi ya wengine. (D. McAllister)

kwa ujumla neno masengenyo limetafsiriwa na wanazuoni kama ifuatavyo:

Kwa mujibu wa Dk. Alison Poulsen anasema kuwa masengenyo ni mazungumzo yasiyo ya lazima au umuhimu na wakati mwingine yenye kutisha dhidi ya watu wengine huku yakihusisha usaliti wa kutoboa siri na kusambaza taarifa potofu au hukumu zenye kuumiza.

Na kwa upande wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la tatu la mwaka 2013 inafafanua kuwa neno masengenyo kuwa ni bughudha, kusemwasemwa na kitenzi sengenya kuwa ni sema mtu kwa ubaya wakati hayupo.

Kwa mantiki hiyo katika  muktadha wa tafsiri ya Kamusi tajwa hapo juu ni kwamba kumsema mtu kwa uzuri wakati hayupo hiyo haiwezi kuitwa masengenyo.

Ili kuelezea ukubwa wa tatizo la masengenyo baadhi ya wataalamu wa masuala ya jamii na saikolojia wameonesha kuwa asilimia 14 katika vijiwe vya kahawa mazungumzo yake huwa ni ya kusengenyana  na asilimia 66 ya mazungumzo kwa wafanyakazi walioajiriwa mada zao za kijamii huwa ni kuwaongelea watu wengine. (Cole and Dalton, 2009)

Hata hivyo bado kuna utata kuelewa chanzo halisi  ambacho husababisha binadamu ambao kimsingi wameumbwa kwa mfano wa Mungu, kupendelea mazungumzo ya kuwaponda wenzao badala ya kuwatamkia mema.

Baadhi ya wanasaikolojia  na wataalamu wengine wanadai kuwa masengenyo wakati mwingine hutumika kuboresha urafiki baina ya wale wanaokutana kwa pamoja na kumzungumzia/kuwazungumzia  mabaya yule/wale ambao hawapo.

Wakati mwingine mtu anaweza kuanzisha masengenyo kama njia mojawapo ya kujionesha kuwa yeye ni mwema na anakubalika  kuliko yule anayemzungumzia  kuwa anao ubaya fulani.

Si tu mtu mmoja mmoja hutumia masengenyo kama mtaji bali pia inaaminika kuwa hata baadhi ya taasisi za kazi masengenyo hutumika kama zana ya kuimarisha mahusiano ya kawaida kwa waajiriwa. (Noon and Delbridge, 1993; Dunbar, 2004; Kniffin and Wilson, 2005)

Maongezi hasi ambayo hutumika katika  taasisi/shirika ili kuwafanyia tathimini wafanyakazi  wengine ambao hawapo huitwa masengenyo hasi. (de Gouveia et al., 2005; Chandra and Robinson, 2010; Wu et al., 2016).

Kimsingi awe ni  msengenyaji, mwenye kupokea masengenyo au yule mwenye kukaa pembeni akiwa kimya huku akisikiliza kinachozungumzwa  ilimradi  wote wamekuwapo katika eneo yalipofanyika masengenyo wakishuhudia, basi kwa namna moja au nyingine watakuwa wameathirika na hilo tukio. ( Rejea chapisho la Asistance employee program)

Mbali na masengenyo kuwa na  madhara  kwa mtu mmoja mmoja, lakini ni hatari zaidi yakifanyika katika  taasisi/shirika   kama ifuatavyo:.

Masengenyo husababisha kutengeneza mazingira ya woga na kutoaminiana baina  ya wafanyakazi kitendo ambacho kinaweza kuchochea chuki na hatimaye kuzaa uadui. Baadhi ya wasomi huamini kuwa masengenyo katika maeneo ya kazi ni aina ya kudumaza jamii ya wafanyakazi waliopo  (Duffy et al., 2002), na wafanyakazi ambao wamezunguka katika maeneo hayo hujikuta ni vigumu kuaminiana na kushirikiana. (Aquino and Thau, 2009

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,464FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles