23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Kwanini simu zinalipuka?

samsung-galaxy-note-7-recall-fire-explosion-3

NA FARAJA MASINDE,

MWAKA huu huenda ukawa si mzuri sana kimauzo kwa kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung kutoka Korea Kusini, hii inatokana na matukio ya mara kwa mara ambayo yanaisababishia hasara kampuni hiyo.

Siku chache zilizopita, Maafisa wa uchukuzi wa ndege nchini Marekani walitoa tahadhari kwa abiria wanaosafiri kwa ndege kutofungulia au kuchaji simu za Samsung Galaxy Note 7 wakiwa ndani ya ndege huku nchi nyingine nazo zikiendelea kuweka masharti kwa abiria wanaotumia simu hizo.

Kampuni ya ndege ya (FAA) pia imewashauri watu kutoweka simu hizo kwenye mizigo wanayoingia nayo eneo wanamoketi abiria kwenye ndege.

Tayari kumeshuhudiwa matukio mbalimbali ya kulipuka kwa simu hizo ikiwamo kuunguza magari na vitu vingine hali iliyosababisha kampuni ya Samsung kuagiza kurejeshwa kiwandani kwa simu hizo kutokana na hitilafu wakati wa uundaji wa betri.

Simu hizo zilidaiwa kulipuka zikiwekwa chaji au baada ya kuwekwa chaji, chanzo cha kulipuka kwa simu hizo kinaelezwa kuwa ni ‘seli’ zilizoko ndani ya betri za simu hiyo.

Kampuni hiyo hata hivyo ilisema ni vigumu kutambua ni simu gani zilizo na kasoro.

Hili linaelezwa kuwa tukio la kwanza kuwa na madhara zaidi kwa kampuni hiyo.

Mashirika ya Australia ya Qantas na Virgin Australia pia yamewashauri wateja kutoweka chaji simu zao au hata kuzitumia wanaposafiri kwenye ndege.

Tayari simu takribani milioni 2.5 za Note 7 zilikuwa zimesambazwa kwenye maeneo mbalimbali duniani.

Wateja walionunua simu hizo walilazimika kuzirejesha ambapo kazi ya kupata simu mpya itachukua takribani wiki mbili.

Awali, Samsung walitangaza kusitisha uuzaji wa simu hizo kutokana na matatizo ya betri, lakini baadaye ziliingia sokoni, na kwasasa wamekiri kwamba hakuna namna simu hizo zina tatizo.

Wakati kampuni hiyo inapitia kipindi hicho kigumu, kampuni ya Apple kupitia simu zake za iphone tayari imeingiza simu mpya sokoni ya iPhone 7.

Apple imekuwa ni mshindani mkubwa wa Samsung kibiashara ambapo inatazamiwa kuuza simu nyingi zaidi za iPhone 7.

Kampuni hiyo imesema kwamba itakuwa vigumu kudhibiti faida mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo mauzo yake yaliongezeka zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles