24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KWA REKODI HII…. DAYNA NYANGE UMETISHA ASIEE

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KAMA ingefanyika sensa ya kuhesabu wasanii kutokana na maeneo wanayotoka basi mkoa wa Morogoro ungeshika nafasi za juu kutokana na ukweli kwamba umekuwa na wanamuziki wengi toka enzi za kina Mbaraka Mwinshehe, Juma Kilaza, Alfosi Maleko na wengineo.

Hata muziki wa Bongo Fleva ulipoanza kupata umaarufu Morogoro, imekuwa mastari wa mbele katika kutoa wasanii ambao wamekuwa na mrejesho chanya kwenye tasnia nzima ya muziki.

Heshima kubwa kwa Suleiman Msindi  ‘Afande Sele’ ambaye amekuwa kama kaka na kiongozi wa kutoa mwelekeo na mawazo yenye maarifa ya kuwajenga wasanii wa kizazi kipya ambao leo wanafanya vyema kwenye Bongo Fleva kutoka Morogoro.

Morogoro ya sasa inawategemea wasanii kama Lameck Ditto, Stamina,Koba, Dayna Nyange, Belle 9 na wengine ambao hawajatoa kazi mpya muda mrefu sasa.

Wasanii wakike ni adimu mno, anayeng’aa kwa sasa ni Dayna Nyange pekee ambaye wiki hii amevunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa  Bongo Fleva kutwaa tuzo ya toka muziki huo uanze kupata mashiko kwenye jamii ya kitanzania.

Dayna ameshinda tuzo ya Brave Afrcan Entertainers (BAE Awards) 2017, zilizotolewa mapema wiki hii nchini Nigeria katika vipengele viwili tofauti ambavyo vilimkutanisha na wasanii kutoka mataifa mbalimbali.

Kipengele cha kwanza ni kile cha Mtumbuizaji Bora wa Kike (Best Vocal Performance Female) kupitia wimbo wake wa Angejua, alishindana na wasanii wa Nigeria kama Aramide, Ngowari na Rocknana.

Pia katika kipengele cha pili cha Msanii Bora wa Kiafrika (Best African Act) ambacho kilikuwa kinawaniwa na wasanii wakubwa kama Eddy Kenzo (Uganda), Rabbit (Kenya), Stonebwoy (Ghana) na Jah Vinci wa Jamaica.

Rekodi…

Ikumbukwe kuwa toka ameanza kufanya muziki hajawahi kushinda tuzo yoyote mpaka hivi majuzi aliposhinda tuzo hizo mbili za kimataifa.

Nakumbuka aliwahi kusema kuwa amewahi kushinda tuzo ndogo huko nyumbani kwao Morogoro na hakuwahi kabisa kushinda nyingine yoyote hivyo tuzo hizi zimekuwa za kwanza kwake na kwa wasanii wote wa Morogoro.

Kwa Afande Sele vipi..

Huyu aliwahi kupata heshima ya kutwaa taji la Mfalme wa Rhymes mwaka 2003. Taji siyo tuzo bali ni heshima ambayo hupewa mtu na jamii fulani iliyotambua mchango wa mtu huyo.

Afande Sele alipewa heshima na familia ya Hip Hop kwa kuwa mchango wake unaonekana wazi kwenye muziki huo na tasnia nzima ya Bongo Fleva.

Belle 9

Staa huyo wa singo ya Give It To Me naye amekuwa na bahati mbaya, mara nyingi mashabiki wamekuwa wakilalamika pale ambapo Belle 9 anaingia kwenye tuzo fulani lakini hafanikiwi kushinda licha ya kuwa na uwezo mkubwa kisanii.

Amewahi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Tanzania (KTMA) zaidi ya mara mbili lakini hakuambulia kitu na mara zote Diamond Platnumz alishinda, kitu kilichosikitisha watu wengi.

Stamina naye..

Rapa mahiri kwenye kizazi hiki, Stamina ni miongoni mwa wasanii wa Morogoro ambao wamekuwa na bahati mbaya ya kutoshinda tuzo licha ya kupenya kwenye tuzo za KTMA lakini akaondoka mikono tupu.

Aliwahi kuwania tuzo kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Hip Hop lakini hakufanikiwa kuchukua ingawa ni rapa mkali katika kizazi hiki.

Hata Lameck Ditto pia

Mwaka 2019 akiwa kwenye kundi la La Familia alishirikishwa na Chid Benz kwenye wimbo unaoitwa Dar es salaam Stand Up. Wimbo ule ulishinda tuzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop.

Licha ya kuufikisha mbali wimbo huo hajawahi kushinda tuzo yake mwenyewe nadhani singo yake hii mpya ya Moyo Sukuma Damu inaweza kumpa tuzo huko tuendako.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles