22.7 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Kwa nini mipango mingi ya mwaka huwa haitekelezeki?

Na CHRISTIAN BWAYA

HERI ya mwaka mpya! Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutujaalia kuingia mwaka mpya 2020.

Kama ilivyo kawaida, wengi wetu huwa tunaanza mwaka mpya kwa msisimko. Tunaweka malengo mapya; wapo ambao huanza mwaka kwa kujiwekea maazimio ya kubadili tabia wasizozipenda; kuanzisha mwenendo mpya wa maisha; kutekeleza malengo fulani ya kijamii na kiuchumi yatakayobadili maisha kwa mwaka unaoanza.

Ingawa ni kweli kwamba mwaka unapoanza kinachobadilika huwa ni tarehe tu, wengi wetu huamini wanaingia kwenye zama za maisha mapya. Imani hiyo huambatana na jitihada za kujaribu kubadili maisha yao yaendane na zama hizo mpya.

Wanasema, ‘mwaka mpya na mambo mapya’ hata hivyo, ni dhahiri kuwa maazimio mengi yanayowekwa wakati mwaka unapoanza, huishia tarehe za mwanzoni mwa Januari. Msisimuko wa mipango mipya, maisha mapya, zama mpya, huishia mwaka ukiwa bado mpya.

Baada ya hapo maisha hurudi kulekule yalikotoka.

Tafiti zinasema asilimia kati ya 8 na 10 tu ya watu wanaoweka malengo ya mwaka mpya, ndio hutekeleza malengo hayo kufikia mwisho wa mwaka. Maana yake asilimia kati ya 90 na 92 huwa wa- naweka maazimio yasiyotekelezeka.

Katika makala haya, tunajadili kwa nini maazimio mengi mazuri hufa kabla hayajaanza kutekelezwa.

MIHEMKO YA KUANZA MWAKA

Kuingia mwaka mpya ni jambo la kusisimua. Watu wengi hutafakari namna wengine walivyoshindwa kuuona mwaka mpya.

Kwamba ‘wamejaaliwa’ huwafanya wajione kama watu wenye wajibu fulani wa kubadili mtindo wao wa maisha yaendane na mwaka wanaouanza.

Msisimko huu, kwa hakika, huwa ndio msingi wa maazimio mengi yanayowekwa wakati wa kuingia mwaka mpya.

Kwa bahati mbaya maazimio yanayoongozwa na msisimko wa namna hii hayawezi kuleta matokeo yoyote ya maana. Sababu ni kwamba msisimko wa kuingia mwaka mpya unapoyeyuka, basi na maamizo nayo huyeyuka na hatima yake mfumo wa maisha unarudi kulekule ulikokuwa.

MALENGO YASIYOPIMIKA

Sambamba na kuweka maazimio katika hali ya msisimko, watu wengi huweka malengo yasiyopimika. Haya ni yale malengo makubwa yanayopendeza masikioni lakini hayana namna ya kutathmini utekelezaji wake.

Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na malengo ya kufanikiwa kwa mwaka unaoanza. Lakini unakuuona mwaka mpya. Kwamba ‘wamejaaliwa’ huwafanya wajione kama watu wenye wajibu fulani wa kubadili mtindo wao wa maisha yaendane na mwaka wanaouanza.

Msisimko huu, kwa hakika, huwa ndio msingi wa maazimio mengi yanayowekwa wakati wa kuingia mwaka mpya. Kwa bahati mbaya maazimio yanayoongozwa na msisimko wa namna hii hayawezi kuleta matokeo yoyote ya maana. Sababu ni kwamba msisimko wa kuingia mwaka mpya unapoyeyuka, basi na maamizo nayo huyeyuka na hatima yake mfumo wa maisha unarudi kule- kule ulikokuwa.

MALENGO YASIYOPIMIKA

Sambamba na kuweka maazimio katika hali ya msisimko, watu wengi huweka malengo yasi- yopimika. Haya ni yale malengo makubwa yanayopendeza masikioni lakini hayana namna ya kutath- mini utekelezaji wake.

Kwa mfano, mtu anaweza kuwa na malengo ya kufanikiwa kwa mwaka unaoanza. Lakini unapomwuuliza ana maana gani anapokusudia kufanikiwa, anakwambia basi tu anataka kufanikiwa.

Lengo hili, la kufanikiwa ni pana mno kwa sababu utekelezaji wake hauwezi kupimwa.

Na kwa sababu ni vigumu kupima utekelezaji wake, ni rahisi kupoteza uzito wake siku chache baada ya kuazimiwa.

KUENDELEZA TABIA ZILEZILE

Utekelezaji wa malengo mengi ni matokeo ya mabadiliko ya tabia. Huwezi kutekeleza lengo la kuweka akiba kila mwezi kama huwezi kubadili tabia ya kufanya matumizi yasiyopangiliwa.

Kwa mfano inawezekana huwezi kuweka akiba kwa sababu unakuwa mwepesi wa kuwapa watu fedha usizokuwa nazo. Unatoa usichonacho kwa sababu huna uwezo wa kusema hapana. Ukiendelea kuwa na huruma isiyo na kiasi ni wazi unakwamisha malengo yako.

Kadhalika, huenda unaishiwa kwa sababu una tabia ya kununua vitu usivyovihitaji. Hata unapokuwa huna fedha unatafuta furaha kwa kununua vitu fulani. Usipoweza kubadili tabia hizi, huwezi kutekeleza malengo unayojiwekea.

Ndio kusema watu wengi huwa hawafikirii namna mambo makubwa yanavyochangiwa na mambo madogo madogo. Na kwa sababu hawaoni mchango wa

mambo madogo katika mambo makubwa ni rahisi kupuuza mambo hayo ambayo kimsingi ndiyo yanayosaidia kuleta mabadiliko makubwa.

Kwa mfano, mtu anayetaka kuacha pombe, anafikiri kile anachotaka kukipata, yaani kuacha pombe lakini hafikirii mchango wa mazingira yanayoambatana
na unywaji wa pombe. Mazingira haya kwa mfano, ni pamoja na kukaa katika maeneo yanayohamasisha unywaji wa pombe na hata kuambatana na wanywaji wa pombe.

Unapoishi na walevi ni vigumu kubadili tabia unayotaka kuiacha. Kuachana na tabia waliyonayo watu wako wa karibu ni sawa na kuwapinga. Si watu wengi wanaweza kukubali kuwapinga watu wao wa karibu.

KUTAFUTA VISINGIZIO

Hakuna binadamu anapenda kujisikia hatia. Hii ni hulka ya mwanadamu. Wengi wetu tunapoona hatuwezi kufanya kitu fulani tunatafuta namna ya kukwepa hatia yao. Mfano, kuwabebesha lawama watu wengine badala ya kuchukua hatua.

Ili uweze kutimiza malengo yako, unahitaji kuwa na kifua cha kuvumilia hatia. Katika safari ya kutimiza malengo, unaweza kufika wakati kile unachokiishi kinaonekana kwenda kinyume kabisa na kile unachokitamani. Usiruhusu kukata tamaa na kuamua kuachana na malengo yako. Unahitaji kuendelea kusimamia kile una- chokiamini hata kama uhalisia unakuwa kinyume.

Kwa mfano, badala ya kuamua kuendelea kunywa pombe kwa sababu tu umerudia tabia hiyo baada ya jaribio la kuacha kwa juma moja, usikate tamaa. Kubali kujisikia hatia na azimia kuendelea kujitahidi kujizuia.

Kukata tamaa mara nyingi hutokana na imani kuwa unapolenga kutekeleza jambo, basi lazima ulitimize kwa asilimia 100. Hakuna malengo hufikiwa kwa asilimia hizo. Kubali kufanikiwa hata kwa asilimia 10 na uendelee mbele. Kuwa na maamuzi yanayoweza kuvumilia kushindwa.

Christian Bwaya ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge (MWECAU). Mawasiliano 0754 870 815

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles