22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

KUWAIT YAMFUKUZA BALOZI WA KOREA KASKAZINI

KUWAIT CITY, KUWAIT

RIPOTI kutoka nchini Kuwait zinasema kuwa itamfukuza Balozi wa Korea Kaskazini, So Chang Sik na wafanyakazi wengine wanne.

Hatua hiyo itabakisha wanadiplomasia wanne tu katika ubalozi huo, ambao haukuweza kupatikana mara moja kuthibitisha hatua hiyo.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa lakini Kuwait imewaambia waandishi wa habari kuwa balozi huyo wa Korea Kaskazini, amepewa mwezi mmoja kuondoka.

Kuwait ndiyo nchi pekee katika ghuba iliyo na ubalozi wa Korea Kaskazini.

Maelfu ya raia wa Korea Kaskazini wanafanya kazi nchini Kuwait na nchi zingine za ghuba kama vibarua.

Hatua hiyo inachukuliwa wiki mbili baada ya kiongozi wa Kuwait kuzuru Washington, Marekani.

Marekani imetaka hatua za kimataifa kuchukuliwa dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia mipango yake ya makombora ya nyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles