27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

KUTANA NA WATOTO WENYE NGUVU ZAIDI DUNIANI

KILA mtoto ana kipaji tofauti na hukionesha kwa njia tofauti. Wakati baadhi wanaweza kuwa wazuri katika uchoraji, wengine hujikita zaidi katika michezo na wachache wengine wakifanya kweli darasani.

Lakini umewahi kusikia au kuona watoto wakifanya yao katika kunyanyua vitu vizito au kujenga mwili kwa mazoezi makali, ambayo watu wazima wasingethubutu kufanya?

Sawa, pengine uko katika mshangao mkubwa au kiasi! Wafuatao  wanahesabika kuwa miongoni mwa watoto wenye nguvu zaidi duniani, ambao watakushtua kwa uwezo na nguvu zao.

1. Giuliano Stroe na Claudiu Stroe

Giuliano Stroe na Claudiu, wenye umri wa miaka tisa na saba bila ubishi ndio watoto wenye nguvu zaidi duniani. Ndugu hawa wawili kutoka  Icoana, kusini mwa Romania, wamekuwa wakinyanyua vitu vizito tangu wakiwa na umri wa miaka miwili na wanaweza kufanya mazoezi ambayo huogopesha hata watu wazima.

Baba yao ni mkufunzi na huwafanya wavulana hao kupitia taratibu zote ikiwamo mlo unaotakiwa na vipindi vya mafunzo kila siku. Giuliano tayari amevunja rekodi ya dunia kwa aina za pushapu.

2. Yang Jinlong

Yang  ana umri wa miaka saba tu na uzito wa 110 lbs sawa na kilo 50, ijapokuwa hafuati utaratibu wa mlo na mazoezi ya kumjenga kama watoto wengine wenye nguvu walioorodheshwa katika makala haya, anastahili kuwamo hapa.

Yang anaweza si tu kumbeba baba yake mwenye uzito wa 200 lbs sawa na kilo 91 mgongoni mwake bali pia anaweza kulivuta gari la familia yao barabarani kwa nguvu yake.  Kwa taarifa 1 lbs ni sawa na kilo 0.453.

Mvulana huyu wa Kichina kwa hakika kwa umri wake huo ni mtoto mwenye nguvu duniani.

3. Richard Sandrak

Akiwa amezaliwa Ukraine, Richard Sandrak ni mtoto mwingine miongoni mwa wale wanaofanya makubwa ambayo watu wazima hawana uthubutu.

Alianza kufanya mazoezi akiwa na umri miaka miwili na alipofikisha miaka sita, alikuwa tayari akinyanyua uzito wa 180 lbs sawa na kilo 81.

Amezama katika mazoezi kila siku kuinama na kuinuka akiwa na vitu vizito mabegani mara 200 na pushapu 600 push-ups zinazomsaidia kuujenga mwili wake. Kwa sasa ana umri wa miaka 23 na mwili uliojengeka mno.

Maryana Naumova

Anahesabiwa kuwa msichana mwenye nguvu zaidi duniani, Maryana Naumova kutoka Urusi amethibitisha kuwa nguvu si sifa kwa wavulana pekee.

Akiwa mnyanyua vitu vizito maarufu, Maryana (16), ni mshindi kwa kila hali. Katika umri wa miaka 15, alishiriki katika onesho la Arnold Classic – mchuano uliopewa jina la mcheza filamu, gavana na mnyanyua vitu vizito wa zamani Arnold Schwarzenegger na kumshangaza kila mmoja wakati aliponyanyua uzito wa 331 lbs sawa na kilo 150!

5. Naomi Kutin

 

Msichana mwingine mnyanyua vitu vizito na umri wa miaka 13, Naomi Kutin. Msichana huyo wa maajabu alivunja rekodi zote wakati wakati alipoweza kunyanyua uzito wa 215 lbs – ambao ni mara mbili ya uzito wa mwili wake – katika umri mdogo wa miaka 10. Naomi hakuishia kushangaza watu na baada ya miaka kadhaa aliweza kunyanyua mabegani  231 lbs na kuinua uzito wa 249 lbs, akivunja zake za awali. Si ajabu anaitwa “msichana wa aina yake”.

. CJ Senter

CJ Senter ni mtoto wa Kimarekani anayeamini katika ujenzi wa mwili na unyanyuaji wa vitu vizito. CJ amekuwa akifanya mazoezi tangu akiwa na umri wa miaka mitano.

Akiwa na umri wa miaka 10, alijipatia umaarufu , aliponekana katika DVD akionesha umahiri wake wakati akionesha namna watoto wanavyoweza kujitengeneza katika umbo la kuvutia.

7. Varvara Akulova

 

Mzaliwa huyu wa Ukraine Varvara Akulova, yu ndani ya kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness akihesabiwa kama msichana mwenye nguvu zaidi duniani. Alianza kunyanyua vizito akiwa na umri wa miaka minne na kufikia umri wa miaka 10, tayari alikuwa na rekodi ya unyanyuzi wa vitu vizito kwa kunyanyua 220 lbs.

Miaka minne badaye alivunja rekodi yake mwenyewe kwa kuinua 660 lbs! akiwa amejaliwa na nguvu za ajabu akiwa ametokea kwa wazazi ambao walifanya kazi katika kikundi cha sarakasi, mwili wake ni mwepesi na hauonekani kuwa na nguvu alizo nazo sasa kwa kunyanyua vizito vya mno.

Jake Schellenschlager

Kwa kuingia katika mazoezi na ujenzi wa mwili katika umri wa miaka 12, mnyanyua vitu vizito Jake Schellenschlager (sasa 15) ni mmoja wa watoto wenye nguvu zaidi duniani. Akiwa na uzito wa 119 lbs katika umri wa miaka 14, Jake alimshangaza kila mmoja kwa kunyanyua 225 lbs katika mchuano huko Pennsylvania. Kana kwamba hilo halitoshi, alienda kunyanyua 300 lbs i.e. uzito wa mara mbili ya ule wa mwili wake. Mvulie kofia mvulana huyu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles