30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

KUTANA NA WATALAAMU WA MASAJI KWA KUTUMIA NYOKA

Joseph Hiza na Mashirika

IWAPO unajisikia kuchoka au kuwa na maumivu, kuna mbinu mbalimbali za kuondoa hali hiyo kupitia masaji.

Aina za masaji ziko nyingi zinaweza kuwa na mbinu kama Shiatsu, Swedish, Thai na ‘Deep Tissue’. Lakini nadhani unaweza kujaribu kitu kipya: tiba ya nyoka.

Je, umewahi kuisikia tiba ya aina hii? Kama ndio au ndio unaisoma hapa je, upo tayari kufanyiwa? Una ubavu au ujasiri wa kukabiliana nayo?

Ni nini hiki lakini? Tunazungumzia masaji ya kutumia nyota wakubwa kama chatu badala ya mikono milaini!

Iwapo una ubavu au ujasiri wa kufanyiwa masaji kwa kutumia nyoka, basi funga safari kuelekea katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Kama unadhani watu wataikimbia huduma hii, utakuwa unajidanganya, kwa vile wengi hujitokeza kiasi cha kupanga foleni kwa saa kadhaa kusubiri zamu yao.

Inapatikana hiyo kituo cha utaoaji huduma mbalimbali kama hizo kijulikanacho kama Bali Heritage Reflexology and Spa kilichomo mjini humo.

Kwa mujibu ya watoa huduma na wateja, huduma hii ina uwezo mkubwa wa kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.

Masaji hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na wengine huachiwa afanye yake mwilini.

Wengi wa watu wanaofanyiwa na masaji hiyo ya aina yake wanaeleza kuifurahia na hawaonekani kuogopa baada ya kuwa na uhakika wa kuwa salama dhidi ya viumbe hao hatari.

Huduma hiyo ya kutumia nyoka inaelezwa kutoa tiba ya aina yake ya masaji ambayo inahusisha kuweka nyoka kadhaa aina ya chatu kuvinjali katika mwili wa mteja.

Mtambao wa nyoka hao wanaovinjali na upumuaji wao unaoweza kusababisha hofu unaelezwa kuleta athari chanya kwa metaboli za mwanadamu.

Wateja jasiri hulipa kiasi cha Dola za Marekani 47 sawa na Sh 96,000 za Tanzania kupata huduma hii ya dakika 90.

Kutokana na kubainika kuwa nyoka watumikao kwa kazi hiyo ya utoaji huduma ni wale wasio na sumu na midomo yao huwa imefungwa, wengi hujitokeza kupanga foleni kusubiri zamu zao kupata tiba hiyo.

Nchini Israel kuna huduma kama hiyo ambayo si tu kwamba inahusisha nyoka bali pia panya ambao inaaminika wanapowekwa mwilini au miguuni mwa mteja huondoa mbinyo na misongo ya siku aliyo nayo.

Ili kuwa na uhakika wa kutomsababishia mteja usumbufu au kitisho chochote, daima nyoka hawa wanalishwa panya hai ili wawe muda wote wa masaji wakiwa wameshiba.

Akiwa amelala katika meza tayari kwa kufanyiwa masaji, Feri Tilukay amefumba macho na kuonekana akitabasamu mara kwa mara wakati nyoka wakubwa watatu walipokuwa wakivinjali mwilini mwake mwote.

Huyu ni mmoja wa wateja wa kawaida wenye ujasiri wa kujaribu ‘masaji ya nyoka’, ambayo badala ya kutumia mikono, ngozi ya mijusi hawa wenye urefu wa mita 1.8 hutumika.

“Huwa najisikia raha ya aina yake kwa kweli,” Tilukay (31) alimwambia mwandishi mmoja wa habari huku nyoka watatu wakimtambaa.

Akiwa amevalia tu kaptura, alionekana akisisimka wakati nyoka hao watatu waitwao Jasmine, Muscle na Brown wakiwa kazini mwilini mwake.

Walikuwa wakimtamba shingoni, wakijizungusha tumboni na mgongoni mwake na mara nyingi wakisugua shingo na kutoa ndimi zao.

Wataalamu wawili huhudhuria pia ili kuhakikisha usalama na kuwachochea nyoka wachangamke kazini, midomo ikiwa imezibwa— watambae huko na kule na kuhakikisha hawakai katika eneo moja tu.

Kabla ya huduma hiyo, nyoka huchukuliwa kutoka maboksi ya plastiki, ambayo huwekwa na kuoshwa na dawa.

Wakati watu wengi ambao wanaenda kupata huduma hiyo kituoni hapo, kuna wengine wanaofika kushuhudia na wengine wengi kama Tilukay wakiijaribu mara ya kwanza.

“Awali nilikuwa nikiwaogopa nyoka. Lakini baada ya kupata tiba ya masaji ya nyoka mara kadhaa, nimeanza kuondokana na woga huo na sasa nawapenda sana viumbe hawa,” alisema Tilukay, ambaye ni mhasibu.

Kijana huyo ni mmoja ya wateja wachache wa Indonesia kwa vile wengi hutokea Ulaya, Japan au Korea Kusini kwa mujibu meneja mkuu wa kituo hicho, Paulus Abraham.

Anasema tiba ya masaji ya nyoka ni moja ya huduma 300 zinazotolewa kituoni hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles