24.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 30, 2022

Contact us: [email protected]

Kutana na wanawake wanaoishi kama midoli

dolsTANGU midoli ianze kutengenezwa katika miaka ya 1950, wasichana bila kusahau wanaume kote duniani wamekuwa wakijaribu kuiga mionekano yao.

Ni kama ajabu vile, wakati watoto wengi wakichezea midoli maarufu kama Barbie, wanawake hawa wanajitengeneza katika mwonekano wa midoli, hali inayowafanya wawe katika kundi la watu wa kushangaza duniani.

Unapowatazama unaweza dhani si watu halisi bali mwanasesere au roboti lenye umbo la mwanadamu.

Lakini amini usiamini katika dunia hii isiyoishiwa na vituko na vijimambo, unayemwona mbele yako ni mtu halisi, aliyejibadili kuwa katika mwonekano huo wa kiuanasesere.

Baadhi yao wameenda mbali zaidi wakiapa kuishi maisha ya mdoli kwa maisha yao yote hapa duniani.

Miongoni mwa majina maarufu zaidi yanye mwonekano wa midoli halisi ni pamoja na Valeria Lukyanova wa Ukraine, Anastasiya pia Ukraine, Rodrigo Alves wa Brazili ambaye hivi karibuni alilazimika kuwekwa pua mpya bandia baada ya awali kunyofoka. Wengine ni pamoja na Angelica Kenova wa Urusi na wengineo wengi.

Wasichana hawa hufuatiliwa na kundi kubwa la wafuasi katika mitandao ya jamii na wamekuwa wakichukua hatua za kuhakikisha wanalinda vilivyo mwonekano wao.

Hutumia vipodozi na upasuaji kwa gharama yoyote kufanikisha hilo.

Hata hivyo katika miaka ya karibuni mionekano hiyo imekuwa ikipigwa vita na wanaharakati mbalimbali kutokana na madhara yanayotokana na upasuaji wa mara kwa mara.

Mbali ya madhara kitendo hicho huvuta wasichana wengi kutamani kuingia katika mkumbo huo wa kujibadili kupata sura na umbo la uanasesere.

Walio katika mkumbo huo ni pamoja na wanawake maarufu wanaolenga kuonekana taswira ya mdoli kuanzia kiuno chembamba, makalio makubwa na macho makubwa.

Ukiacha na upasuaji huo waliofanyiwa, wanadada hawa hutumia muda wao mwingi kukaa katika vioo vyao wakijipodoa, kutengeneza macho yao yawe na muonekano wa midoli halisi.

Kwa mfano, Anastasiya ambaye alianza kufanyiwa upasuaji tangu akiwa na umri wa miaka 18 yeye hutumia zaidi ya dakika 30 kwa jicho moja tu, kulichora na kulipaka vitu anavyovijua yeye mwenyewe ili apate muonekano ule wa mdoli.

Licha ya kufahamika wengi wao hufanyiwa upasuaji, kinara katika midolo hiyo hai, akijulikana mdoli anayeishi, Valeria Lukyanova (31) amekuwa akikana mara kwa mara kufanyiwa upasuaji.

Bila aibu husema kwamba kubadilika kwake kutoka taswira ya awali hadi ya sasa inatokana na upangiliaji wa mlo na mazoezi.

Mwanamitindo huyo wa Ukraine, DJ na mwimbaji mara ya kwanza alitengeneza vichwa vya habari miaka mitatu iliyopita baada ya picha zake zikionesha kiuno chembama kusambaa mitandaoni.

Mashabiki wake waliamini kwamba alifanyiw upasuaji kuwa na mwonekano huo kutokana na wanavyomfahamu tangu ashinde moja ya mataji ya urembo duniani mwaka 2007.

Lakini Valeria alisisitiza kwamba kulinganishwa na mdoli kumetokea tu kwa bahati na kwamba ni tusi kudai ameiga taswira ya mdoli.

Alidai kwamba umbo lake limetokana na mlo mzuri unaohusisha pamoja na samaki na juisi ya matunda na mazoezi mengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles