KUSOMA NCHI ZA NJE KUNASAIDIA KUJIFUNZA MENGI

0
765
Abdulmalik Mollel akizungumza na wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma nje ya nchi

Na ASHA BANI  


        

SERIKALI ipo katika harakati za kuhakikisha nchi inakuwa na uchumi wa viwanda utakaosaidia kukuza pato la Taifa na hata kuongeza ajira kwa vijana.

Lakini haya yote hayawezi kufanyika bila kuwapo kwa elimu ya uhakika yenye kiwango kinachostahili ambacho Watanzania watawekeza katika kuendeleza Taifa lao.

Kwa Tanzania pekee, haiwezi kuwa na uwezo wa kutoa elimu ya vyuo vikuu pasipo kushirikisha mataifa mengine ya nje ili kuhakikisha wakufunzi wanaozaliwa wanakuwa wa kiwango cha juu katika kusaidia na kukuza maendeleo ya nchi.
Tanzania kwa sasa ipo katika nafasi nzuri katika ukuaji wa Sayansi na Teknoloji na ni kutokana na kwamba wataalamu wengi wanaokwenda kusoma nje wenye uzalendo hurudisha nchini utaalamu wao na kusaidia taifa.

Hapa ndipo Kampuni ya Uwakala ya wanafunzi wanaotaka kwenda kuosoma vyuo vikuu vya nje ilipoanzishwa mwaka 2006 ijulikanayo kwa jina la Global Education Link (GEL) ikiwa chini ya  mwasisi na mwanzilishi wake Abdulmalik Mollel.

Mollel ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo ambaye anasema kuwa alipokuwa anasoma nje aliona utofauti wa mambo mengi kielimu kati ya vijana wa Kitanzania hasa katika suala zima la kutafuta fursa mbalimbali kupitia elimu.

 

Katika makala haya Mollel anaeelezea kwa kina sababu ya kuanzisha GEL shughuli zake, vyuo wanavyopeleka wanafunzi sifa na manufaa ya kusoma nje kwa kutumia kampuni yake ya uwakala.

Anasema ilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha inawasaidia Watanzania kuwapa maelezo sahihi kuhusu vyuo vya nje na mwongozo mzima kuhusiana na uchaguzi sahihi wa masomo. 
Mollel anasema kuwa  endapo mwanafunzi atakwenda kusoma nje kwa kusaidiwa na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na uratibu  na usimamizi kwamba anasafiri vipi atafikia wapi ataishi vipi na atasoma nini ni lazima mwanafunzi huyo atafanikiwa.

Anasema kampuni hiyo imekuwa na usimamizi wa kumwangalia mwanafunzi na si kumpelekea na kumwacha akihangaika kama wanavyofanya mawakala wengine aliowaita kuwa ni kama matapeli.
“Sisi tumeamua kufanya hivyo ili kuepuka Mtanzania anapokwenda kusoma akiwa peke yake anaweza akapatwa na matatizo na mzazi akashindwa kwa kupata msaada wa mtoto wake amsaidiaje, lakini sisi tunaratibu mwanzo hadi mwisho wa safari yake na masomo pia hadi atakapomaliza,’’anasema Mollel.

Anasema wazazi wengi wamekuwa wakishindwa kufanya utaratibu wa watoto wao kusoma vyuo vinavyoeleweka na matokeo yake hupatwa na matatizo mbalimbali kwa kuwa wanashindwa kufahamu utamaduni wa nchi husika anayokwenda.

Anayataja matatizo hayo kuwa ni pamoja na kushindwa kupata visa ndani ya siku 14, uthibitisho wa nchi na chuo anachokwenda kama kinatambuliwa na bodi za vyuo vikuu katika nchi husika kama kinakiwango ambacho pia kitaendana na kiwango cha Tanzania.

Anasema GEL katika nchi ambazo wanapeleka wanafunzi  kusoma wanakuwa na mawasiliano na balozi za Tanzania ambapo mwanafunzi akipatwa na matatizo inakuwa ni rahisi moja kwa moja kuwasiliana na kupata msaada wa haraka.

Anasema mtandao walionao husaidia wazazi kufahamu matokeo ya mwanafunzi na kama atakuwa amefanya vibaya au amekuwa na tabia mbaya ambayo inaweza kuiharibia sifa nchi haraka anarudishwa nchini.

“Tayari wanafunzi saba wamerudishwa nchini katika kipindi cha mwaka huu kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu, tunafanya hivi ili asije kuharibu sifa ya nchi na kuambukiza tabia mbaya kwa wanafunzi wengine.

 

“Mara kwa mara tumekuwa tukishirikiana na wazazi kwa kufanya mikutano ya mara kwa mara na kuanzisha magroup ya mtandao wa WhatsApp wazazi kupewa nyilwa ‘password’ ya kuingia katika mtandao atakaoweza kumfuatilia mwanafunzi atakapokuwa nje ya nchi,” anasema Mollel.

Mollel licha ya mafanikio katika kazi yake hiyo, anaelezea changamoto anazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na wazazi kufahamu tabia mbaya za watoto wao  lakini anampeleka  kusoma nje akidhani kuwa ni njia ya kumpunguzia mzigo.

Anataja changamoto nyingine kuwa ni wazazi kushindwa kulipia tiketi, malazi na chakula. Wakati mwingine hukwama kulipa ada.

Mollel anasema huwapeleka wanafunzi hao katika kozi mbalimbali ikiwamo kusomea mambo ya petroli na gesi, kozi za biashara, masoko, afya, udaktari, madini na uchumi.

Anataja baadhi ya shule wanazowapeleka kuwa ni China, Malaysia, India, Canada, Marekani, Australia, Uingereza, Afrika Kusini na Ukraine. 
Anataja sifa za wanafunzi kuwa ni wale waliomaliza kidato cha nne, sita na vyuo mbalimbali nchini. 
Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa imeweza kuwaunganisha Watanzania zaidi ya 5400 na vyuo mbalimbali duniani.

Akiizungumzia GEL, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako anasema kazi wanayoifanya ni nzuri.

Naye Balozi wa India nchini, Sandeep Arya anasema GEL ina usimamizi mzuri kwa wanafunzi kutoka Tanzania wanaokwenda kusoma nchini humo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here