LONDON, UINGEREZA
UPIGAJI kura bungeni kuhusu makubaliano na Umoja wa Ulaya (EU) juu ya mchakato wa Uingereza kujiondoa rasmi kutoka umoja huo, maarufu kama Brexit utafanyika Jumanne ijayo.
Awali mwezi uliopita Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May alilazimika kuahirisha kura hiyo baada ya kukiri kuwa mpango wake huo ungeshindwa.
Licha ya kutangaza mchakato huo, May alisema Uingereza itajikuta mahali pagumu iwapo mpango wake na Ulaya utakataliwa.
Hadi sasa dalili zinaonesha hajaweza kuwashawishi wabunge wenye msimamo mkali kuunga mkono mpango wake.
Uingereza inatarajiwa kuondoka rasmi kutoka Umoja wa Ulaya Machi 29 mwaka huu.