23.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Kupe janga jingine Uingereza

LONDON, UINGEREZA

WATU nchini Uingereza wameombwa kuwa katika tahadhari baada ya ugonjwa usio wa kawaida unaosambaa kwa kuumwa na kupe kubainika kwa mara ya kwanza nchini humo.

Wizara ya Afya imesema hatari iliyopo kwa umma ni ya chini lakini ni muhimu wawe waangalifu kuhusu kupe hasa wanapokuwa kwenye maeneo ya bustani msimu wa joto.

Imeelezwa kuwa ugonjwa huo unasababishwa na vimelea ambavyo vinaathiri chembe nyekundu za damu.

Tayari mgonjwa wa pili aliyeambukizwa ugonjwa huo ambao ni nadra sana kutokea amegunduliwa.

Ugonjwa huo unaosambazwa na kupe unaosababisha ubongo kufura mara nyingi hutokana na maambukizi ya virusi.

Dk. Katherine Russell kutoka Wizara ya Afya nchini humo amesema ugonjwa huo ni nadra sana na hivyo basi uwezekano wa maambukizi ni wa chini mno.

“Kupe hupatikana sana kati ya msimu wa kuchipua na pukutizi, kwahiyo ni muhimu ikiwa raia watachukua tahadhari ya juu ili kuhakikishi hawaumwi na kupe wanapokuwa nje wakijivinjari. Na pia tafuta ushauri wa daktari unapoanza kusikia vibaya baada ya kuumwa na kupe,” alisema Dk. Katherine.

Wizara ya afya imesema imepima mamia ya kupe katika eneo la Devon karibu na anapoishi mgonjwa wa kwanza aliyebainika na ugonjwa huo, lakini wote hawakupatikana nao.

Na pia vipimo vya damu kutoka Hampshire katika maeneo karibu na anapoishi mgonjwa mwingine vimeonekana kuwa salama.

Wagonjwa wote wanapata matibabu hospitalini na kulingana na Kituo cha Kuzuia Magonjwa Ulaya kimesema ugonjwa huo unasambazwa tu na kupe ambao hupata maambukizi kwa kuumwa na ng’ombe walio na maambukizi na panya buku.

Kuna watu 39 waliothibitishwa kupata maambukizi barani Ulaya, nje ya Ulaya, ugonjwa huo mara nyingi hutokea Marekani.

DALILI

Watu wengi wenye ugonjwa huo ama hawatakuwa wanaonesha dalili au dalili za maambukizi ni za wastani. 

Hata hivyo, watu wenye mfumo wa kinga ya mwili dhaifu wanaweza kuumwa sana, wakilalamikia dalili za kama mafua, homa, kuhisi baridi, kuumwa na misuli, uchovu na homa ya nyongo ya njano.

Karibia theluthi mbili ya watu wenye maambukizi ya ugonjwa huo hawataonesha dalili, kwa walio na mafua na homa, kuumwa kichwa na uchovu wanaweza kupata ugonjwa wa utando wa ubongo au kufura kwa ubongo na kupooza mwili.

Shingo inapokakamaa na kuumwa kichwa, kupata maumivu kwa kuangalia mwanga wa taa, kuzimia, kuwa na mabadiliko ya tabia- kama kuchanganyikiwa ghafla na kuhisi baadhi ya sehemu za mwili zinashidwa kusongea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,437FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles