24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kupatwa jua kwafungua lango hifadhi ya Ruaha

Kupatwa kwa jua.
Kupatwa kwa jua.

Na Upendo Fundisha,Mbarali

WAKATI leo dunia ikitarajiwa kuelekeza macho yake mkoani Mbeya kushuhudia kupatwa kwa jua kitufe, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),  limetangaza kutumia tukio hilo kufungua lango la Ikoga katika Wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya kuongeza watalii katika Hifadhi ya Taifa Ruaha

Kufunguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa.

Akizungumzia hatua hiyo jana, Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),  Pascal Shelutete, alisema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa  eneo la Ihefu   lina kivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Mfune, alisema wilaya hiyo ina vivutio vingi.

Aliwataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua leo hii kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea leo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana katika Kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya.

Maeneo mengine yatakayoshuhudia tukio hilo la historia ni wilaya za Ludewa na Wangong’ombe mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wataalamu,  tukio hilo lilitokea nchini kwa mara ya kwanza mwaka 1977  na linatarajiwa kutokea tena mwaka 2032.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, aliwataka wananchi wanaotaka kushuhudia tukio hilo kuhakikisha wanatumia kifaa maalumu pamoja na miwani   kuepuka madhara ya kuugua macho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles