29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Kunenge ushirikiano mlionipa Dar mumpatie na Makala

Na Brighiter Masaki

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambae kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge leo May 19 amekabidhi ofisi kwa Mkuu Mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala,, ambapo amewashukuru Watumishi wote wa Mkoa huo kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati wa uongozi wake.

Kunenge amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa Imani kubwa aliyomuonyesha kwa kumteua kuongoza Mkoa wa Pwani.

Aidha Kunenge amesema ushirikiano wa kazi baina yake na watumishi wote wa Mkoa viliwezesha kupatikana kwa mafanikio makubwa.

“Nitoe wito kwa watumishi wote wa Dar es Salaam kuendelea kumpa ushirikiano mliokuwa mkinipa mumpatie na Mkuu wa Mkoa mpya ili aweze kutimiza maono ya Rais Samia Katika Mkoa huo.”

Kwa upande wake Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala amempongeza Kunenge kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya katika mkoa huo na kueleza kuwa anaamini uwezo alioonyesha Dar es Salaam ataupeleka Mkoa wa Pwani.

Makabidhiano ya ofisi yamefanyika mbele ya viongozi wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wastaki Meya, Viongozi wa Usalama, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakuu wa Idara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles