26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kunenge aagiza wanafunzi nane wafukuzwe sekondari

Na BRIGHITER MASAKI – DAR ES SALAAM 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakari Kunenge ameagiza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Pugu  Stesheni, kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafukuza  wanafunzi nane kwa utovu wa nidhamu.

Akizungumza wakati wa ziara yake shuleni hapo jana, Kunenge alisema dhumuni la ziara hiyo ni kutatua changamoto za shule hiyo, ikiwamo idadi kubwa ya wanafunzi na ukosefu wa maji.

 “Kazi ya walimu ni wito, nawaomba wazazi kuwalea watoto katika mazingira mazuri, wafuate misingi imara  ili kujenga vijana bora watakaoweza kulisaidia taifa,” alisema Kunenge.

Alisema ni kosa wanafunzi wa shule kuhatarisha usalama wa shule na mali zake.

“Taarifa ya Mkuu wa Shule hii, Simoni Lupogo inaeleza kuwachukulia hatua wanafunzi wanane kwa utovu wa nidhamu,  nimetoa kibali uongozi wa shule yenu kuwachukulia hatua ili kuisafisha shule hiyo iwe safi,” alisema Kunenge.

Aliagiza wafukuzwe wanafunzi wote wenye utovu wa nidhamu mara moja ili shule iwe safi iweze kupandisha kiwango cha taaluma.

Wakati huo huo, Kunenge alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Janeth Stephen  kuweka ulinzi katika shule hiyo kwa walimu wote na wanafunzi  kuwahakikishia usalama wakati wote.

Amemtaka Kamanda Janeth   kuhakikisha ulinzi unakuwepo shuleni hapo kutokana na kundi linalohatarisha usalama kwa kushiriki vitendo viovu.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Elzabeth Thomas alikiri kuzipokea changamoto za shule hiyo na kuzitatua kwa wakati ikiwemo kuweka uzio wa shule na ununuzi wa kompyuta.

Mkuu wa Sekondari ya Pugu Stesheni, Lupogo alisema uongozi wa shule hiyo umewachukulia hatua wanafunzi nane kwa kosa la uvutaji bangi na kuhatarisha usalama wa shule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles