25.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Kundi lililojhihami Sudan lashambulia kijiji kimoja Darfur na kuwauwa watu 7

DARFUR, SUDAN

KIKOSI maalumu cha kijeshi nchini Sudan kimewashambulia raia katika eneo la Kusini mwa jimbo la Darfur. 

Watu saba wameuawa na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa. 

Taarifa hii imetolewa na wanaharakati katika eneo hilo pamoja na kundi moja la waasi katika eneo hilo linalokumbwa na machafuko.

Mashambulizi hayo yametokea wiki moja baada ya kundi la kujihami linalohusishwa na serikali kuvamia kambi moja Kaskazini mwa Darfur na kuwauwa watu 13.

Msemaji wa kundi la waasi linalojiita vuguvugu la ukombozi wa Sudan Abdel-Rahman al-Nayer, amesema shambulizi la hivi punde zaidi lilifanywa siku ya Alhamisi na watu waliokuwa wamejihami waliowafyatulia risasi watu waliokuwa wakielekea katika mashamba yao katika mji wa Gereida umbali wa kilomita 107 Kusini mwa Darfur.

Ghasia katika jimbo la Darfur zinahatarisha uthabiti wa kisiasa katika serikali ya mpito. 

Mnamo mwezi Aprili mwaka jana, vuguvugu linalotaka demokrasia lilimuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir na kuanzishwa serikali ya mpito inayowajumuisha viongozi wa kijeshi na kiraia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,444FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles