Kundi la Mtu Chee kuundwa upya

0
948

young deeNA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kuwa kimya kwa miaka miwili, kundi la muziki wa hip hop nchini, Mtu Chee, linatarajiwa kurudi kwa kasi kubwa katika tasnia ya muziki.

Kundi hilo linaloundwa na wasanii Boniventure Kabogo, ‘Stamina’, Ibrahim Mandingo ‘Country Boy’ na David Genzi ‘Young Dee’, linarudi baada ya maombi ya wadau mbalimbali wa muziki nchini.

Kwa niaba ya wenzake, Country Boy alisema wameshaanza kurekodi kwa prodyuza Rash Don studio ya Kiri Record, ili kurudisha upya kundi hilo lililowahi kutamba na wimbo wa ‘Mia’ ambao ulitengenezwa na prodyuza Manecky.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here