30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kuna upungufu wa wahandisi wanawake’

Mhandisi Steven Mlota
Mhandisi Steven Mlota

 

NA FLORIAN MASINDE, DAR ES SALAAM

SERIKALI imesema kuna upungufu mkubwa wa wahandisi wanawake unaochangia kuongeza changamoto katika sekta ya uhandisi nchini.

Hayo yalibainika jana jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Uhandisi Tanzania kitengo cha wahandisi wanawake.

Akizungumza katika mkutano huo Msajili wa wahandisi nchini, Mhandisi Steven Mlota, alisema hapa nchini kuna upungufu mkubwa wa wahandisi wanawake kulinganisha na wanaume na kusababisha changamoto kubwa katika kuongezea idadi yao ili kuendana na mahitaji ya sekta zinazotegemea wahandisi.

“Kwa sasa ni asilimia nane tu ya wahandisi wanawake ambapo 13 kati yao ni wale waliobobea na 319 ni wataalamu wa masuala ya uhandisi kwa hiyo kunahitajika mikakati madhubuti kuweza kuongeza idadi yao kwa kuwa ni watu muhimu sana katika kufanikisha mipango mbalimbali ya Serikali,” alisema Mhandisi Mlota.

Aliongeza kuwa miaka mitano iliyopita, Serikali ya Norway kupitia ubalozi wake nchini ulitoa shilingi bilioni tatu kufadhili na kuwajengea uwezo wahandisi wanawake ili waweze kusajiliwa na Bodi ya Wahandisi.

“Nipende kuishukuru Serikali ya Norway kwa kuendelea kufadhili kitengo hiki ambapo awali walitoa shilingi bilioni tatu kwa muda wa miaka mitano na sasa wametoa zaidi ya bilioni nne kuwawezesha wahandisi wanawake ili kufikia vigezo vinavyotakiwa,” alisema Mlota.

Naye Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema Serikali inatambua mchango wa wahandisi nchini hasa wanawake lakini kunahitajika juhudi na mikakati madhubuti ili kuongeza idadi ya wahandisi.

Alisema kwa kutambua umuhimu wao katika maendeleo ya nchi hasa katika sekta za nishati, madini, barabara, maji na kilimo, Serikali inaendelea kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuongeza vyuo vya uhandisi na kufikia tisa.

“Licha ya idadi hiyo ya vyuo ni vyema kuongezea ushawishi kwa watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati na kudahiliwa katika vyuo vinavyofundisha fani ya uhandisi,” alisema Samia.

Aliongeza kuwa kwa sasa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeagiza kuwa masomo ya sayansi yatakuwa ni lazima na si hiari kama ilivyokuwa awali na yatakuwa yanafundishwa kuanzia kidato cha tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles