Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA
WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema bado kuna uhaba wa mbegu wakati ni taji 186,000, zinazopatikana sasa ni tani,57,000.
Kauli hiyo, aliitoa jijini Dodoma jana,wakati akizundua mkakati wa kuendeleza zao la mpunga awamu ya pili.
Alisema wakulima wamekuwa wakilima kilimo cha hasara na kudai mikakati ni kuhakikisha wengi wanalima kilimo cha biashara.
Alisema sababu ya kutowapo mbegu zenye ubora na uchache wa mbegu maeneo mengi nchini, yanasababisha wakulima kukata tamaa.
Alihoji mbegu bora zipo wapi,wakulima wamekuwa hawazipati hivyo uzalishaji kupungua.
“Mbegu bora zipo wapi? na wanaozalisha wapo wapi? ifike mahali mbegu zizalishwe hapa hapa,Rais Dk.John Magufuli alisema ni aibu kuagiza mbegu nje ya nchi, mimi nasema hili halikubaliki,”alisema.
Alionesha kushangazwa na mbolea kutoka nje ya nchi na kuwataka wote wanaohusika kulisimamia hilo.
“Kwanini tuagize mbolea kutoka nje, tunashindwa kuwa na viwanda hata viwili tu, mbolea za jumla si nzuri,zimepitwa na wakati,”alisema.
Alitaka mikakati iwekwe kutokana na wakulima kupoteza mazao wakati wa uvunaji.
Alisema malengo waliyojiwekea, ni kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga kutoka tani milioni 1.1 mwaka 2018 hadi tani milioni 2.2 mwaka 2030.
Alisema mikakati iliyopo, ni kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora,kulima kisasa,kupunguza gharama za uendeshaji na kuimarisha masoko kwa wakulima wadogo wadogo.
Katika hatua nyingine,Waziri Hasunga alisema ni jambo la kushangaza mikakati kuandaliwa kwa lugha ya Kiingereza wakati wanaoenda kuitumia ni Watanzania ambao wengi hawajui lugha hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Mathew Mtigumwe alisema Serikali imejipanga kuendeleza kilimo cha mpunga.