28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Kuna haja kubadili mfumo wa ulaji, kuepuka magonjwa

CHRISTINA GAULUHANGA – DAR ES SALAAM

KADRI siku zinavyokweda, ndivyo magonjwa ya kila aina yanavyozidi kuongezeka.

Ongezeko la magonjwa hayo inadaiwa huenda inasababishwa na ulaji au unywaji wa vyakula vyenye kemikali.

Sasa hivi ugonjwa wa kisukari umekuwa tishio hadi kwa watoto wadogo, hali inayodaiwa kusababishwa na mfumo wa maisha.

Siku hizi, biashara ya vyakula na vinywaji vingi vimekuwa vikichanganywa na kemikali, na hata mazao shambani yamekuwa yakiwekwa dawa na viuatilifu.

Sababu hizo na nyinginezo huenda ndio chanzo cha kukithiri kwa magonjwa mbalimbali katika jamii.

Ukiangalia bibi na babu zetu miaka ya zamani walikuwa wakitumia vitu vya asili na waliishi hadi miaka 100 tofauti na sasa ambapo ni nadra kumkuta mtu mwenye miaka 50 hajaanza kushambuliwa na maradhi.

Asilimia kubwa ya vijana na hata wazee utasikia wanasumbuliwa na maradhi ya miguu, shinikizo la damu, sukari na mengineyo.

Wapo baadhi ya watalaam na asasi zinazoshughulika na masuala ya tiba mbadala au kilimo hai  kama Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai nchini (TOAM), ambao wamekuwa wakishauri kutumia vyakula vya asili ili kujenga afya.

Hii ni kwa sababu vinaweza kusaidia kupunguza magonjwa ambayo ni tishio katika jamii na humaliza nguvu kazi ya taifa.

Ifike wakati, jamii itafakari upya na kuona ni wapi tulipoangukia ili tusijikwae tena, ni muhimu kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya vyakula vyenye kemikali kwa mustakhabali wa maisha yetu.

Ni vema familia zikabadilika taratibu na kupunguza kiwango cha kemikali na hata mafuta ili kuondoa magonjwa haya yanayoshambulia watu wengi na kusababisha wengine hata kupoteza uwezo wa kufanya kazi zao za kila siku.

Ulaji mzuri wa vyakula, vinywaji na hata matunda yasiyo na kemilikali unaweza kukuweka sehemu salama zaidi tofauti na kutumia vitu vyenye kemilika.

Vitu vya kioganiki vinatumia zaidi malighafi zinazotuzunguka kwenye maeneo tunayoishi hivyo haviwezi kumgharimu mzalishaji au mfanyabiashara.

Wakati ni sasa wa familia kubadilika na kutumia vitu vinavyozalishwa kioganiki ikiwamo vinywaji, vyakula, mafuta ya kula, kupaka na hata sabuni.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles