22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Kumbukizi miaka 20 kifo cha Nyerere wiki hii

PATRICIA KIMELEMETA

WADAU kutoka taasisi za dini na makundi mbalimbali wanatarajia kushiriki kwenye kongamano la kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Wadau hao, pamoja na mambo mengine, watajadili mchango wa mwananchi katika kuleta maendeleo ya taifa na mtu mmoja mmoja.

Kongamano hilo, limeandaliwa na Chama cha Wanataaluma Wakatoliki Tanzania (CPT), litafanyika Mei 16,mwaka huu jijini Dar es Salaam litajadili kwa kina  maendeleo jumuishi na yenye kujali ustawi wa maisha ya wananchi.

Akizungumza na   MTANZANIA jijini Dar es Salaam  jana, Mratibu wa CPT, Mariam Messy alisema watajadili sera zenye uwiano sawa kati ya mzalishaji na mpokeaji kutokana na ukuaji wa uchumi hasa katika kipindi hiki ambacho serikali inatekeleza mpango wa uanzishwaji wa viwanda.

Alisema kutokana na hali hiyo, ukuaji wa uchumi utakua kwa kasi jambo ambalo linaweza kuwanufaisha wananchi wote bila kuangalia tofauti zao.

Alisema licha ya uchumi kukua, lakini pia wananchi wanapaswa kuelimishwa ili waweze kuona umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili iweze kuwafikia wengi na kuleta tija katika jamii zao.

“Katika kipindi hiki ambacho serikali inatekeleza mpango wa kuanzishwa viwanda, wananchi wanapaswa kuelimishwa ili waweze kujiunga na kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo itawasaidia katika maisha yao baadae,” alisema Mariam.

Aliongeza kuwa kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi unaendelea nchini,wananchi wanapaswa kuelimishwa kuu ya kujiunga na huduma za kifedha ili viweze kuwafikia wengi zaidi mijini na vijijini.

Alisema anaamini kongamano hilo, linaweza kuleta matokeo chanya kwa wananchi, jambo ambalo linaweza kusaidia ukuaji wa uchumi.

Zaidi ya maaskofu watano na maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), wanatarajiwa kushiriki kwenye kongamano hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles