23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kumbilamoto kuzindua klabu ya mpira Yongwe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa klabu ya mpira wa miguu (Yongwe FC) iliyopo Chanika.

Katibu wa Yongwe FC, Rashidi Mtimbande, amesema wameandaa bonaza kwa ajili ya uzinduzi wa klabu hiyo litakalofanyika Agosti 7 kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Yongwe.

Amesema wameanzisha klabu hiyo ili kuibua vipaji vya vijana na kuvikuza pamoja na kushiriki mashindano mbalimbali ya ngazi ya wilaya, mkoa hadi taifa.

“Tayari tumefanikiwa kupata usajili wa klabu yetu na sasa tunajiandaa katika mashindano mbalimbali ngazi ya wilaya na mkoa kwa sababu michezo ni ajira,” amesema Mtimbande.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Klabu hiyo, Abdallah Haule, amesema kwa sasawana timu mbili ambapo ya watu wazina ina wachezaji 32 wakati timu ya vijana ina wachezaji 19.

Hata hivyo amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa vifaa vya michezo na kuwaomba wadau kujitokeza kuwasaidia.

“Kuna vijana wengi wanapenda kucheza mpira lakini unapokuwa na timu inatakiwa iwe hata na mipira mitano lakini ina mpira mmoja, unafanya mazoezi wengine wako matumbo wazi, kiwanja tunachotumia nacho hakina nyavu,” amesema Haule.

Mmoja wa wachezaji wa timu ya vijana, Vitalis Kimea (15) amesema anapenda mpira na malengo yake ni kuja kuwa mchezaji mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles