24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘KULENI MATUNDA KUEPUKA VICHWA VIKUBWA’

Na LILIAN JUSTICE -MOROGORO

WANANCHI mkoani Morogoro wametakiwa kula matunda na vyakula vyenye virutubisho vya madini ya foliki, ili kupunguza ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Tawala, Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, alipokuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi, yaliyofanyika mjini hapa.

Alisema kwamba tatizo la kuwa na kichwa kikubwa na mgongo wazi linaepukika, kama wananchi watakuwa mstari wa mbele kula matunda, yakiwamo machungwa na mapapai.

Pia, alisema matatizo hayo yatakwisha kama wananchi watatumia vidonge vyenye vitamin ya foliki, ambavyo husaidia kwa kiwango kikubwa kuzuia tatizo hilo.

“Binafsi nashangaa kuona Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye tatizo hilo, licha ya wananchi wake kuzalisha matunda kwa wingi.

“Kwahiyo, nawaomba wananchi wale matunda kwa wingi badala ya kuyauza kama inavyofanyika sasa,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi Wenye Watoto Wenye Ulemavu wa Kichwa Kikubwa na Mgongo Wazi (ASBAHT), Abdulhakim Bayakub, alisema pamoja na kufanya jitihada za kusaidia watoto hao kwa matibabu, bado hazifanikiwi zaidi kutokana na ukubwa wa gharama za matibabu hayo.

“Gharama za vipimo ni kubwa, kwani mtoto akiwekewa mpira inagharimu kiasi cha shilingi laki tano.

“Chama cha ASBAHT kimekuwa kikishirikiana na hospitali zote ambazo matawi yake yapo, lakini bado tunahitaji msaada wa wadau wenye uwezo wa kufanya hivyo,” alisema.

Awali, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Rita Lyamuya, alisema kliniki zote zinapaswa kutoa vidonge vyenye vitamini ya foliki acid, ambavyo vinawasaidia wajawazito kujifungua bila matatizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles