22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Kuhamia Dodoma kutakuza huduma zinazotumia teknolojia

g6

NA FARAJA MASINDE,

TAYARI Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, imeweka wazi azma yake ya kutaka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.

Dodoma ni miongoni mwa miji inayopiga hatua katika suala zima la maendeleo nchini licha ya ukweli kuwa ukuaji wake bado hauwezi kulinganishwa na miji mikubwa kama, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.
Uamuzi huo wa serikali ambao awali uliwekwa wazi na Rais Dk.John Magufuli ni kichocheo kikubwa cha kukua kwa huduma zinazotumia teknolojia kubwa na za kisasa kwenye mji huo ambazo utekelezwaji wake unategemewa kukua kwa kasi kubwa zaidi.

Unapozungumzia suala zima la maendeleo hasa ya miji ni wazi kuwa huwezi kuiacha sekta ya ujenzi ambayo kwasasa ndiyo imekuwa kitovu kikubwa cha ustawi wa miji duniani kote kupitia teknolojia za majengo ya kisasa.

Hivyo hili liko wazi kabisa kuwa makao makuu haya ya nchi yanatarajiwa kupendezeshwa zaidi na taswira za majengo ya kisasa ambayo yatakuwa na faida lukuki zikiwamo za serikali kuyatumia kama moja ya ofisi zake, maduka ya kisasa,hoteli, achilia mbali makampuni ya teknolojia yatakayowekeza kwenye majengo hayo kwa ajili ya kufunga mitambo ikiwamo pia huduma za Intanet.

Licha ya ukweli kuwa teknolojia za majengo ya kisasa ikiwamo ile ya kusafisha vioo vya majengo makubwa aina ya Rope Access kuchelewa kufika nchini lakini ni ukweli kuwa Tanzania inafanya vizuri katika ujenzi wa majengo ya kisasa.

Ukiachilia mbali teknolojia ya majengo eneo jingine ambalo linatarajiwa kukua zaidi ni lile la usafiri wa anga ambapo ndege kubwa zitakuwa na uwezo wa kutua Dodoma.

Siku chache zilizopita, Waziri Mkuu Majaliwa alizindua upanuzi wa uwanja wa ndege wa mkoa huo unaotarajiwa kujengwa kisasa kwa kuhusisha teknolojia zinazokwenda na wakati kwa sababu utakuwa ukitumiwa na viongozi na mabalozi wa nchi mbalimbali na wafanyabiashara iwapo mpango wa serikali wa kuhamisha makao makuu utakamilika.

Maoni, ushauri|0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles