25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kuchanganya dawa za kienyeji, kisasa ni hatari’

Na DERICK MILTON-SIMIYU

KUTUMIA dawa za kienyeji na za kisasa kwa wakati mmoja kunasababisha madhara makubwa kutokana na dawa hizo kuwa na sumu tofauti, hivyo kuathiri mwili kwa kiasi kikubwa.

Kati ya madhara makubwa yanayotokea kwa mtu ambaye anachanganya dawa hizo, ni pamoja na kuharibika kwa figo, ini, kupata matatizo ya moyo, na kupanda kwa sukari.

Hayo yalisemwa jana na daktari bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Harun Nyagori katika mkutano wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waandventista Wasabato (ATAPE) mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Profesa Nyagori aliwataka wagonjwa kutochanganya dawa hizo.

Suala la afya ni moja ya huduma zinazotolewa na chama hicho.

“Watu lazima watambue kuwa dawa za kisasa asilimia 75 zinatokana na miti shamba na hiyo miti ina sumu ya kuharibu wadudu kwenye mwili, na dawa za kienyeji nazo zina sumu pia, sasa ukichanganya hizo sumu zikakutana ndiyo madhara yanakuwa makubwa,” alisisistiza Profesa Nyagori.

“Tunawashauri watu wakiamua kutumia dawa za kisasa wasichanganye na za kienyeji, wakiamua za kienyeji wasichanganye na kisasa, lakini pia tunawashauri wakitaka kutumia za kienyeji wafanye utafiti kwanza kujua kiwango cha sumu kilichomo,” aliongeza daktari huyo bingwa.

Aidha Profesa Nyagori alisema toka mkutano huo umeanza siku mbili zilizopita, watu 269 wamepimwa, na 103 kati ya hao wamekutwa na tatizo la shinikizo la damu huku 62 wakikutwa na tatizo la sukari.

 Mwenyekiti wa ushirika wa maji ATAPE (Life Water Project), Elias Marwa, alisema chama hicho kinategemea kuchimba visima 25 vya maji nchi nzima.

Mbali na visima, alisema wanatarajia kuanzisha kiwanda kikubwa cha maji katika Mkoa wa Kilimanjaro ili kuunga mkono sera ya Serikali ya viwanda. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles