27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kubenea: Sitomfuata Mwambe CCM

ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema),  amesema katika Uchaguzi Mkuu 2020 kila anayechaguliwa ndiye anatakiwa kutangazwa ili kuepuka vurugu zisizokuwa za lazima kama miaka iliyopita.

Pia amesema hawezi kuhama Chadema kumfuata aliyekuwa Mbunge wa Ndanda,  Cecil Mwambe ambaye alitangaza kukihama chama hicho wiki iliyopita na kujiunga na CCM.

Hayo aliyasema juzi Dar es Salaam wakati wa mkutano wake wa hadhara wa jimbo uliofanyika Ubungo Kibo, ambapo alisema uchaguzi ili uwe wa haki anayeshinda ndiye anatakiwa kutangazwa na si vurugu za kutakiwa kutumia nguvu kubwa.

Kubenea alisema licha ya CCM haitaki kuwepo na tume huru ambayo itasimamia uchaguzi ulio huru na wa haki, lakini ndiyo ilikuwa suluhisho kubwa la kuwa na uchaguzi wa haki ambapo mshindi halali anatangazwa.

 â€œTume ya uchaguzi ilikuwepo tangu mwaka 1985, wakati huo kulikuwepo na mfumo wa chama kimoja, lakini sasa ni mfumo wa vyama vingi, lazima kuwepo na mabadiliko hayo, si vyema kukawepo na mfumo ambao unapendelea chama kimoja.

“Mwalimu Nyerere alituachia umoja, uhuru, mshikamano, hivyo lazima tuuenzi, lazima kuwepo na tume huru, uchaguzi huru na watu wake wawe huru ili kuwepo na amani,’’ alisema Kubenea.

Akizungumzia kuhusu kuhama chama hicho kama ambavyo wengi wamekuwa wakitabiri baada ya kuondoka kwa Mwambe, alisema si kweli hawezi kumfuata.

“Siwezi kumfuata Mwambe ingawa alikuwa rafiki yangu wa karibu sana, lakini si lazima niende alipokwenda yeye, na kama ningekuwa kwenda basi nilishakwenda tangu wakati wa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, Fredrick Sumaye.

“Lakini pia CCM nina marafiki zangu wengi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na kaka yangu Bernard Membe, lakini sijafikiria hilo, ndio ije leo kwa Mwambe?’’ alihoji Kubenea.

Naye Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amelalamikia hatua ya kuminywa kujisimamia kufanya kazi za halmashauri wenyewe na badala yake kuharibiwa mipango yao ya maendeleo.

Alitolea mfano mwaka 2015-2106 walikuwa wakisimamia miradi mbalimbali, mfano ya barabara na hata kama kuna barabara mbovu kunahitajika fedha ilikuwa wakitoa kwa urahisi na kufanyika kwa ujenzi kwa usimamizi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles