26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Kubenea: mchakato kumng’oa Meya Dar si halali

Asha Bani, Dar es Salaam

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema) amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana kuacha kutumika katika harakati za kumtoa Meya wa Jiji hilo, Isaya Mwita katika nafasi yake.

Kubenea amesema hayo leo Ijumaa Januari 17, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la meya huyo.

Kubenea ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha ya jiji, amesema uamuzi uliofanyika kwenye kikao kilichofanyika jana Januari 16 si halali kwa kuwa kimeendeshwa kinyume na utaratibu wa kisheria.

“Kikao cha juzi kilifanyika chini ya dakika tano mbele ya askari pia hakikwenda sawa na wala hawakupata muda wa kujadili matumizi ya fedha mbalimbali za halmashauri na mpango kazi haukupitiwa,” amesema.
Amesema kutokana na hali hiyo, maamuzi ya juzi yaliyofikiwa ya kikao cha kamati ya fedha si halali kwa sababu kikao kimeendeshwa kinyume na utaratibu.

Hata hivyo, Liana alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kama wajumbe hawajaridhika na maamuzi hayo waende ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemia) kulalamikia hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles