Kubenea kuwashtaki polisi kwa Msajili, Spika

0
862
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea akimkabidhi Katibu ya Mburahati vifaa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwemo mihuri na vitabu kwa ajili ya kusoma na kuelewa taratibu za uchaguzi

Asha Bani, Dar es Salaam

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amesema anatarajia kuandika barua kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwaelezea jinsi anavyozuiliwa na Jeshi la Polisi kufanya mikutano na shughuli za chama katika jimbo lake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Jumapili Oktoba 20, Kubenea amesema alilalamikia hatua ya kuzuiwa mikutano na wananchi ili kufanya mambo ya maendeleo.

“Kama Msajili na Spika wa Bunge hawatasikiliza kilio hicho basi atakishawishi chama chake kwenda Umoja wa Mataifa kuelezea yanayotukabili ikiwa ni pamoja na kunyimwa kufanya mikutano na wananchi wetu,” amesema.

Katika hatua nyingine, mbunge huyo aligawa vifaa kwa ajili ya uchaguzi wa serikali ya mitaa ikiwa ni pamoja na vitabu na mihuri katika kata 46 za jimbo hilo.

Amesema hata kama Jeshi la Polisi wanawafifiisha katika kufanya kazi lakini watahakikisha wanashinda uchaguzi wa serikali za mitaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here