31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Kubenea kizimbani tena

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (46), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusambaza habari ya uongo yenye kichwa cha habari “Yuko wapi atakayeiyokoa Zanzibar”.

Kubenea alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, akikabiliwa na shtaka la kutangaza habari za uongo ambazo zingeweza kupeleka hofu kwa jamii katika gazeti la Mwanahalisi.

Akisoma hati ya mashtaka jana, Wakili wa Serikali, Dereck, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Willbroad Mashauri,alidai Kubenea alifanya kosa hilo Julai 25,mwaka huu Mtaa wa Kasaba Wilaya ya Kinondoni.

Mukabatunzi alidai Julai 25, mwaka huu, mshtakiwa alisambaza habari ya uongo kwenye gazeti la Mwanahalisi  la kati ya Julai 25-31,2016,  toleo namba 349, ISSN 1821-5432 yenye kichwa cha habari “Yuko wapi atakayeiyokoa Zanzibar”.

Alidai  habari ama makala hiyo ingeweza kusababisha  hofu kwa jamii ama kuharibu hali ya amani.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Kubenea alikana na upande wa mashtaka ulidai   upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na ukaomba kesi iahirishwe hadi tarehe nyingine itakayopangwa na mahakama kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Jopo la mawakili wanaomtetea Kubenea likiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya na Faraji Mangula liliomba apatiwe dhamana kwa sababu shtaka linalomkabili linadhaminika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles