27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KUBENEA AKOMALIA TUME HURU

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA


MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), ameomba mwongozo bungeni akidai kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilagi, amelidanganya  Bunge kwa kudai kuwa kuna tume huru ya uchaguzi.

Madai hayo aliyatoa jana wakati akiomba mwongozo bungeni.

Alisema juzi wakati wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu alisimama na kuzuia shilingi kwa maelezo ya waziri kuhusiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

“Kwamba Serikali ilete mabadiliko ya sheria yatakayofanya tume ya taifa ya uchaguzi kuwa chombo huru na kinachoaminika miongoni mwa jamii.

“Sasa Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisimama akasema kuna kesi ipo mahakamani inayojadili Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa msingi huo jambo hilo haliwezi kujadiliwa bungeni.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelipotosha Bunge, ameingilia kazi za Bunge, kesi iliyopo mahakamani ni kesi namba 6 ya mwaka 2018 inayoomba tafsiri ya ushiriki wa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi.

“Na mimi jana(juzi) nilitoa mfano kwamba ilikuwapo kesi ya  katiba ya ‘kuchallenge’ Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na serikali ilileta muswada bungeni wakati kesi ipo mahakamani ya kuunda sheria mpya ya magazeti na kupata habari na sheria hizo zimejadiliwa ndani ya bunge hili na zimepita .

“Lakini pia orodha ya kesi ambazo zilikuwapo mahakamani na Serikali ikaendelea na kazi  zake za kutunga sheria ni pamoja na kesi ya Bunge Maalumu la Katiba ambayo ilikuwa inaomba tafsiri na kesi ya viongozi wa Chama cha CUF.

“Bunge  halikuzuiwa kupokea wabunge wengine walioletwa na upande mwingine ingawa kuna kesi ipo mahakamani. Kama kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itachukuliwa ndiyo msingi katika Bunge hili.

“Ibara ya 97 (5) imeeleza masharti ya kutunga sheria ndani  ya bunge, suala la kesi kuwa mahakamani siyo suala la hilo jambo.

Akijibu muongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Murtaza Giga,  alisema anachoona yeye hiyo ni tume huru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles