27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kuanzishwa bima ya mazao wakulima kufanya kilimo chenye tija

Elizabeth Kilindi, Njombe

WAKULIMA mkoani Njombe wamesema kuanzishwa kwa bima ya mazao kutawafanya kufanya kilimo chenye tija ambacho kitawafanya kupiga hatua kiuchumi kutokana na kutokuwepo kwa hasara zilizokua zinajitokeza hapo awali.

Hayo yamesemwa juzi mara baada ya uzinduzi wa wakala mkuu wa bima hiyo Mtewele General Traders ambapo mmoja wa wakulima Grace Sambala alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata wakati mgumu wanapokutana na majanga kama ya ukame, mafuriko, wadudu na mengine.

“Ni majanga mengi tunayokutana nayo mfano ukame kwa mfano mvua inaweza ikanyesha halafu ikasimama kwa kipindi kirefu lakini pia tunaomba bima hii ije itolewa hata kwenye mifugo,”alisema Grace.

Awali akifafanua juu ya namna ya kujiunga na bima hiyo ya majanga, Mratibu wa Shirika la Bima la Taifa-(NIC) Prosper Peter, alisema ni majanga ya ukame, mafuriko, mvua za mawe na mengine mengi katika kilimo cha mahindi na mpunga ndio waliyoanza kutoa bima.

“Mwaka 2017 Serikali na taasisi zake ilikuja na mpango huu wa kuhakikisha tunatengeneza huduma ya bima ambayo itaenda kuwanufaisha wakulima pamoja na wafugaji. Kwa hiyo mkulima akipata hasara ambayo inatokana na haya majanga na ikathibika basi huyo yuko radhi kufidiwa,”alisema Peter.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa Taasisi ya (TAPBDS), Rahim Manji, ambao ndiyo waratibu wa mafunzo kwa wakulima na mauzo ya bima pamoja na Sady Mwang’onda kutoka Kampuni ya Mtewele general Traders ambao ndiyo wakala wa mikoa ya Njombe, Ruvuma walisema ujio wa huduma hiyo unakwenda kumaliza changamoto zulizokuwa zikiwatesa kwa muda mrefu.

“Sisi kama mtewele General Traders kwa kushirikiana na wenzetu kwa hapa Njombe pamoja na Ruvuma sisi ndio tutakuwa wasambazaji au watoa huduma wa hii bima ya mazao,”alisema Mwang’onda.

“Tupo kwa ajili ya kuona umuhimu wa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kwa kuwa mkulima huyu mara nyingi akilima huwa anasubiri anaomba mungu”alisema Manji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles