24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kroos aitoa Ujerumani ubingwa Euro 2020

MUNICH, UJERUMANI

KIUNGO wa kati wa timu ya taifa ya Ujerumani, Toni Kroos, amesema timu hiyo haina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Euro 2020.

Mchezaji huyo ambaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid, amedai uwepo wa wachezaji wengi chipukizi unawatoa kwenye nafasi hiyo kwa kuwa wengi wao hawana uzoefu mkubwa jambo ambalo litakuwa gumu kwao.

Tayari wababe hao wa soka wamefanikiwa kufuzu kushiriki michuano hiyo baada ya ushindi wa mwishoni mwa wiki iliopita wa mabao 4-0 dhidi ya Belarus huko Monchengladbach.

Kocha wa timu hiyo Joachim Low, amekuwa akiwapa nafasi wachezaji vijana kutokana na wakongwe kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018, lakini Kroos ni mmoja kati ya wachezaji wakongwe waliobaki kwenye kikosi hicho, hivyo mchezaji huyo anaamini wana kazi kubwa ya kufanya.

“Ukweli ni kwamba wachezaji wengi wa kikosi cha sasa hawana uzoefu na michuano hiyo ya Euro, lakini siku zinavyozidi kwenda kuna mabadiliko yanaonekana.

“Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo tutajua nini cha kufanya kutoka na vile tutakavyokuwa, lakini kwa sasa siwezi kuhesabu kuwa sisi ni miongoni mwa timu zenye nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini hiyo haimaanishi kuwa hatuwezi kuchukuwa ubingwa,” alisema mchezaji huyo.

Kwa upande mwingine beki wa kati wa timu hiyo Matthias Ginter, alifanikiwa kupachika bao moja kwenye ushindi huo na kuwa bao lake la kwanza tangu aanze kuitumikia timu hiyo mwaka 2014 huku akiwa amecheza jumla ya michezo 29.

“Kufunga bao nikiwa kama beki wa kati ndani ya taifa langu ni jambo la kujivunia, hii imenionesha kuwa hakuna kinachoshindikana baada ya kucheza michezo 29, lakini kumbe tatizo ni muda,” alisema beki huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles