KOZI ZITAKAZOKUPATIA AJIRA YA KUDUMU AUSTRALIA

0
2211

Na Joseph Lino,

WANAFUNZI wengi wa kimataifa hupendelea kuishi katika nchi walizosoma baada ya kuhitimu masomo kwa ajili ya maisha bora na uzoefu wa taaluma.

Wahitimu wengi wa kimataifa huanza kufanya kazi wakiwa na kibali cha muda ambacho kinaruhusu mwanafunzi kufanya kazi kwa kipindi maalumu.

Kibali cha kazi cha muda kinakuwa ni ngazi ya kupata kibali cha kudumu (Permanent Residency) nchini Australia.

Kwa upande wa Australia, wanafunzi ambao wanakibali cha kudumu pamoja na familia zao wanaweza kubakia nchini humo na kufanya kazi.

Baadhi ya wanafunzi wanapata shida kupata kibali cha kazi cha kudumu kutokana na kozi na kazi kutokidhi mahitaji ya kibali cha kudumu.

Hii inaweza kuwa kosa kubwa kama inavyojulikana kwamba elimu ya juu nchini Australia ni gharama kwa wanafunzi wa kimataifa.

Kwa hiyo, wanafunzi ambao wanataka kukidhi mahitaji ya kupata kibali cha kudumu baada ya masomo wanatakiwa wawe na vigezo kadhaa vya taaluma katika ajira ambazo zinauhitaji mkubwa wa wataalamu nchini humo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Austraria ilitoa orodha ya ajira zenye uhitaji mkubwa katika taaluma.

Wanafunzi wa kimataifa ambao wamemaliza kozi zenye uhitaji mkubwa katika soko la ajira wanakuwa katika nafasi nzuri za kupata kibali cha kazi cha kudumu.

Kwa hiyo wanafunzi wanaweza kuchagua chuo chochote ambacho kinatoa kozi zenye kuhitajika katika ajira, hata hivyo orodha hiyo huwa inabadilika mara kwa mara.

Kwa maana hiyo inakuwa vigumu kwa wanafunzi wa kimataifa kuchagua taaluma sahihi ya kuwasaidia kupata kibali cha kazi cha kudumu.

Hizi ni baadhi taaluma ambazo hutajika katika soko la ajira na zaidi kulipa mshahara mzuri nchini humo pamoja na nchi nyinginezo. 

Uhandisi

Australia inahitaji wahandisi katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja uhandisi wa meli, kemikali, usafiri, umeme, elektroniki, viwanda, mitambo, madini na mafuta. Nyingine ni kilimo, mazingira. 

Uhasibu

Kusoma uhasibu si jambo rahisi ila ni dhahiri  baada kuhitimu inauhitaji mkubwa wa ajira duniani.

Australia inahitaji wanataaluma katika maeneo mbalimbali ya uhasibu kama usimamizi wa hesabu na kodi.

Vyuo vikuu kadhaa nchini Australia hutoa kozi kuhusiana na uhasibu.

Kwa kuwa vyuo vikuu vya binafsi pia hutoa kozi hizi,  wanafunzi wa kimataifa lazima wawe makini wakati wa kuchagua aina ya kozi ya uhasibu anaoutaka.

Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Uhasibu kwa jumla huwa inasimamiwa na taasisi ya uhasibu nchini humo ya CPA Australia na Taasisi ya Wahasibu katika vyuo vikuu.

Ukifanikiwa kamaliza uzamili wa Usimamizi wa Uhasibu, huandaa wanafunzi wa kuomba kujiunga na Taasisi ya Wahasibu ya Australia (ICAA) au (CPA). 

Uuguzi

Ili kufanya kazi ya uuguzi unapaswa kujua afya ya watu. Australia inauhitaji mkubwa  wa wataalamu wa uuguzi. Kwa ajira ya uuguzi itabidi uwe na ujuzi wa mawasiliano, uvumilivu na ushirikiano katika kazi.

Wauuguzi katika maeneo mbalimbali wanahitajiwa nchini Australia lakini unahitaji kujisajili katika taasisi zinazosimamia sekta hiyo.

Madaktari

Ukosefu wa upatikanaji wa madaktari hugharamu karibu Dola za Marekani milioni 500 kila  mwaka, hii inaonesha ukubwa wa uhaba wa madaktari nchini Australia.

Kusomea daktari nchini humo ni gharama kubwa. Hivyo, kama kweli unataka kusomea kazi hiyo na dawa inahitaji kuwa na fedha za kutosha kwa ajili elimu na baada ya kuhitimu unakuwa na nafasi nzuri ya kuajiriwa na kupata kibali cha kudumu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here