24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Kourtney Kardashian ajirudisha kwa Younes Bendjima


LOS ANGELES, MAREKANI

BAADA ya miezi sita kupita tangu mwanamitindo Kourtney Kardashian na Younes Bendjima kuachana, inadaiwa kwamba mrembo huyo mwenye umri wa miaka 39, amerudisha penzi lake kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 25.

Wawili hao waliachana tangu Agosti mwaka jana, baada ya kuwa pamoja kwenye uhusiano kwa miezi 22, lakini baada ya hapo wakadai wataendelea kuwa marafiki na si wapenzi tena.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, mrembo huyo ameonekana sehemu mbalimbali akiwa na kijana huyo kwa mahaba, hivyo ikimaanisha kwamba wamemaliza tofauti zao na sasa ni wapenzi tena.

Hata hivyo, Jumanne ya wiki hii mastaa hao walionekana wakiwa kwenye mgahawa huko Los Angeles na baada ya kutoka walikuwa wameshikana mikono na kuingia kwenye gari moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles