25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

KORTINI KWA WIZI WA GARI, SIMU

5446974_477x349

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Bunju, Ally Rajabu (29), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Boniface Lihamwike, Mwendesha Mashitaka, Philomena Nchimbi, alidai mtuhumiwa alifanya makosa hayo Novemba 9, mwaka huu, eneo la Kibamba, jijini Dar es Salaam.

“Katika shitaka la kwanza, mtuhumiwa Ally, maeneo ya Kibamba wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, aliiba gari aina ya Suzuki yenye namba za usajili T 724 DHZ, yenye thamani ya Sh milioni 38, mali ya Muba Richard.

“Pia katika shitaka la pili mtuhumiwa katika maeneo hayo hayo ya Kibamba aliiba fedha taslimu shilingi 700,000 na simu mbili, Tecno J8 yenye thamani ya shilingi 350,000 na Tecno C9 yenye thamani ya shilingi 390,000 mali ya Hashim Ally, kwa kujua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za nchi,” alidai Philomena.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, mtuhumiwa alikana kuhusika na wizi huo, hivyo kuambiwa kuwa kosa hilo linadhaminika, awe na wadhamini wawili na mmoja wao atalazimika kusaini bondi ya ardhi yenye thamani ya Sh milioni 38.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 29, mwaka huu, itakaposomwa tena mahakamani hapo na mtuhumiwa amerudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles