22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kortini kwa tuhuma za kununua machangudoa

BETRIDA MWASAMBALILA NA FERDNANDA MBAMILA (DMCT)
WATU wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Jiji kwa tuhuma za machangudoa katika eneo la Buguruni Rozana jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa hao waolifikishwa jana katika mahakama hiyo ni Antidius Severian (25), Yaham Mihamed (24), Ally Hassan (35) na Mohamed Hamis (27).
Wakisomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Bernard Mpepo, alidai kuwa Februari 14, mwaka huu katika eneo la Buguruni Rozana watuhumiwa hao walikamatwa na askari mwenye namba E.7882D/CPL wakifanya manunuzi ya madada poa hao huku wakijua ni kosa kisheria.
Hata hivyo, washtakiwa hao walikana kosa hilo, ambapo Hakimu Mpepo, alisema dhamana kwa watuhumiwa hao ipo wazi ambapo aliwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini dhamana ya Sh 200,000.
Watuhumiwa hao walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Februari 24, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.
Katika kesi nyingine, mtuhimiwa Hassan Mapogilo na wenzake 13 walipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa kosa la kubugudhi abiria katika Kituo cha Mabasi Ubungo.
Akiwasomea hati ya shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Talsira Kisoka, wakili wa Serikali, Ramadhan Kalinga, alidai kuwa mnamo Februari 16 katika eneo la Ubungo waliwabugudhi abiria huku wakiwalazimisha kupanda gari.
Watuhumiwa walikana shtaka hilo na Hakimu Kisoka aliwataka kuwa na wadhamini wawili kwa kila mmoja au kusaini bondi ya Sh 300,000 ambapo walishindwa masharti ya dhamana hiyo na kurudishwa rumande.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles