Kortini kwa kuosha vipimo vya corona vilivyotumika

0
296

Indonesia

Polisi nchini Indonesia imewakamata wafanyakazi wa Kampuni ya dawa ya serikali nchini humo kwa madai ya kuosha vifaa vya kupimia puani ugonjwa wa Covid 19.

Takriban abiria 9,000 katika uwanja wa ndege wa Kualanamu nchini Indonesia huenda wamepimwa Corona na vijiti vya pamba vilivyotumiwa na abiria wengine.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali Kimia Farma sasa inakabiliwa na kesi itakayofunguliwa kwa niaba ya wasafiri.

Mwenendo wa kupima abiria puani umekuwa kama kawaida katika nchi nyingi zilizoathiriwa na janga la Corona.

Polisi wanaamini ulaghai huo ulianza tangu ,mwezi Disemba 2020 katika uwanja wa ndege wa Kualanamu huko Medan, Sumatra Kaskazini.

Mamlaka ya uwanja wa ndege zimekuwa zikitumia vifaa vya vipimo vya Covid-19 vilivyosambazwa na kampuni ya serikali ya Kimia Farma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here