22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

KORTINI KWA KUJIPATIA FEDHA KWA UDANGANYIFU

law-portal

BRIGHITER MASAKI (TSJ) NA MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM

MKAZI wa Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, Evelyne Kasera (43), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na kosa la kujipatia Sh milioni 70 kwa njia ya udanganyifu.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Frank Moshi, Wakili wa Serikali Ramadhan Mkimbu, alidai tukio hilo lilitokea Julai 26 na Septemba 5, mwaka maeneo ya Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam.

Wakili Mkimbu alidai mtuhumiwa alijipatia kiasi hicho cha fedha kupitia akaunti namba 049201045640 inayoonyesha jina la Said Athuman katika benki ya NBC kwamba angemuuzia nyumba namba 2079, Kitalu C iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

“Mtuhumiwa anadaiwa kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia isiyo halali huku akitambua kwamba ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai Wakili Mkimbu.

Baada ya kusomewa maelezo hayo mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo na Hakimu Moshi alisema kwa mujibu wa sheria shtaka hilo linadhaminika, hivyo alimtaka mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili kutoka taasisi inayotambulika kisheria au serikalini.

“Pia kati ya wadhamini hao lazima mmojawapo awe na hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi cha fedha kilichoibwa,” alisema hakimu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 24 mwakani na mtuhumiwa aliachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles