31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yarusha makombora

Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye

SEOUL, KOREA KUSINI

WAKATI mkutano wa mataifa 20 tajiri (G20) ukiendelea nchini China, Korea Kaskazini kwa mara nyingine imerusha makombora ya masafa marefu kinyume na amri ya jumuiya ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Jeshi la Korea Kusini, taifa hilo la kikomunisti lilirusha makombora matatu ya masafa marefu baharini saa chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kukutana na mwenzake wa China, Xi Jinping pembezoni mwa mkutano wa kilele wa wakuu wa G20.

Park alitoa wito wa kuwapo ushirikiano zaidi na China, ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini, kuhusu kile alichosema uchokozi wa mara kwa mara wa Pyongyang.

Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio ya mabomu ya nyuklia na makombora ya masafa marefu mara kwa mara kinyume na makatazo ya Umoja wa Mataifa (UN).

Vyombo vya habari China vimesema Xi amesisitiza kupinga mpango wa Marekani wa kutaka kujenga mfumo wa kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.

Amesema mpango huo huenda ukazidisha uhasama zaidi eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles