Korea Kaskazini yapiga marufuku kejeli

0
937
Kim Jong-un
Kim Jong-un
KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un

BEIJING, CHINA

KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amepiga marufuku raia wa nchi hiyo kutumia kejeli na vijembe katika mazungumzo yao ya kila siku.

Vyanzo vya habari nchini humo vilisema kuwa hakutakuwa na msamaha kwa kejeli zinazoelekezwa kwa utawala wa kikomunisti na hata ukosoaji usio wa moja kwa moja kwa uongozi huo.

Mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na mamlaka za Serikali ilitumika kutoa maonyo hayo.

“Maofisa wa usalama waliendesha mkutano wa kuwatahadharisha wakazi dhidi ya uwezekano wa kutokea matendo ya kihasama yanayoweza kuchochewa na waasi.

“Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ‘kufunga midomo’,” kilisema chanzo cha habari katika Jimbo la Jagang linalopakana na China kwa sharti la kutotajwa.

Chanzo cha habari katika jimbo hilo, kilisema kuwa ujumbe kama huo ulitolewa katika mkutano uliofanyika Jimbo la Yanggang Agosti 28.

Miongoni mwa maneno yaliyoharamishwa na Kim Jong-un ni pamoja na ‘haya yote ni sababu ya makosa ya Marekani.’

Chanzo hicho cha habari kiliongeza: “Tabia hii ya mamlaka kuu kulaumu matatizo ya nchi kwa kutupia wengine kama Marekani kumesabisha uongo kila mahali na kusababisha raia kukikejeli chama cha kikomunisti.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here