KOREA KASKAZINI YALIFANYA JARIBIO KOMBORA LA MASAFA MAREFU

0
1136

SEOUL, KOREA KUSINI

KWA mara nyingine taifa dogo lakini jeuri la Kikomunisti la Korea Kaskazini limefanya jaribio la kombola la masafa marefu licha ya kukatazwa na jumuiya ya kimataifa.

Jaribio hilo limezua shutuma kutoka pande zote za dunia, ambapo Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe, ikiongeza kuwa Pyongyang imechwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu sasa.

Rais mpya wa Korea Kusini, Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini akikitaja kama kitendo cha uchochezi.

Jeshi la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo lilirushwa karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika Bahari ya Japan.

Moon ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri wake wa kiusalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here