22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

KOREA KASKAZINI YALAANI UKOSOAJI WA MAREKANI

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI


KOREA Kaskazini imelaani ukosoaji wa Marekani kuhusu rekodi yake ya haki za binadamu wakati juhudi za kidiplomasia baina ya mataifa hayo zikishika kasi.

Juhudi hizo zinatarajia kuwakutanisha katika mkutano wa kihistoria kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un na marais wa Korea Kusini na Marekani, Moon Jae-in na Donald Trump.

Ripoti ya karibuni iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inaituhumu Korea Kaskazini kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Ukiukaji huo ni pamoja na mauaji ya kiholela, mateso, misako mikali dhidi ya wapinzani na hata kutekwa nyara kwa raia wa kigeni.

Lakini Korea Kaskazini imeipinga ripoti hiyo ikisema inaichafulia jina, na kuituhumu Marekani yenyewe kwa kuwa kitovu cha ukiukaji wa haki za binadamu.

Kim anatarajia kukutana na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in katika eneo la mpakani lisilokuwa na shughuli za kijeshi ijumaa wiki hii.

Baada ya hapo kati ya mwezi ujao na Juni atakutana na Trump katika mkutano wa kihistoria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles