27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yafyatua kombora jipya

PYONGYANG, KOREA KASKAINI

JESHI la Korea Kusini limetoa taarifa kuhusu jaribio la kombora jipya la masafa mafupi aina ya cruise dhidi ya meli, lililofanywa na jeshi la Korea Kaskazini.

Sambamba na Ofisi ya Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kusisitiza kwamba linafuatilia kwa karibu hali ya mambo, imesema kuwa Wizara ya Ulinzi na vyombo vya intelejensia vya nchi hiyo, vitadumisha mashauriano kuhusiana na suala hilo. 

Hata hivyo taarifa zaidi kuhusiana na majaribio ya kombora hilo la Korea Kaskazini bado hazijatolewa.

Mwaka uliopita, Serikali ya Pyongyang na baada ya kuvunjika mazungumzo kati yake na Marekani ilifanya majaribio ya silaha zake mara 13. 

Katika uwanja huo, mwishoni mwa mwaka jana Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini alisisitiza kuwa mlolongo wa majaribio ya makombora yanayofanywa na nchi hiyo ni onyo kwa mazoezi ya kijeshi ya pamoja yanayofanywa na Korea Kusini na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles