28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kaskazini yadaiwa kuua

SEOUL, KOREA KUSINI

VYOMBO vya habari vya nchini Korea Kusini jana vimeripoti kwamba Serikali ya Korea Kaskazini imemuua mjumbe wake maalumu kwa ajili ya Marekani, Kim Hyok Chol, kufuatia kushindwa kwa mkutano wa pili wa kilele kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un na Rais Donald Trump. 

Kwa mujibu wa gazeti la Chosun Ilbo la Korea Kusini, Chol, aliyeuandaa mkutano huo wa mjini Hanoi nchini Vietnam na kumsindikiza Kim kwenye treni yake binafsi, ameuawa kwa kupigwa risasi kwa kile kinachotajwa kumsaliti kiongozi huyo wa juu baada ya kufanikiwa kuishawishi Marekani wakati wa majadiliano ya kabla ya mkutano huo wa kilele. 

Gazeti hilo lililonukuu chanzo ambacho hakikutambulishwa limesema Chol aliuawa Machi, katika uwanja wa ndege wa Mirim pamoja na maofisa wanne waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje baada ya uchunguzi. 

Mkalimani wa Kim kwenye Umoja wa Mataifa naye ametiwa kizuizini baada ya kufanya makosa kwenye mkutano huo wa kilele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles