25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

Kontena laangukia magari saba

Pg 1Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

WATU watatu wamejeruhiwa vibaya na magari saba kuharibiwa katika ajali iliyotokea jana eneo la Tabata, Dar es Salaam.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea baada ya lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 463 DBR na tela yenye namba T 713 AMD lililokuwa kwenye mwendo kasi kupoteza mwelekeo.

Walisema lori hilo lililokuwa linafukuzana na lori jingine aina ya Scania, lilisimama ghafla baada ya kukutana na daladala iliyokuwa ikiingia barabarani kutoka katika kituo kilico jirani na taa za kuongozea magari.

“Yalikuwa magari mawili aina ya Scania ambayo yalikuwa yanafukuzana, yalipovuka taa za kuongezea magari, ghafla kukawa na daladala inaingia barabarani, na kufanya lori lililokuwa kulia likiwa na kontena kujaribu kusimama likiwa kwenye mwendo kasi, hivyo kuyumba na kupoteza mwelekeo.

“Baada ya lori lile kufunga breki ghafla, ilishindikana na kupoteza mwelekeo na kasha kontena lilifyatuka na kuangukia magari madogo yaliyokuwa barabarani na kuyaharibu vibaya,” alisema Imrani Musa.

Alisema katika tukio hilo, dereva wa lori hilo ambaye jina lake halikufamika mara moja alijeruhiwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia aliyekuwa ndani ya gari lake dogo alivunjika mguu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Lucas Mkondya, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Alisema katika tukio hilo watu watatu walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao na kukimbizwa Hospitali ya Amana kwa matibabu.

Kamanda Mkondya alisema lori hilo baada ya kuyumba, kontena lake liliserereka na kwenda kugonga magari mengine saba.

“Magari saba yaliharibiwa vibaya kutokana na kontena kugonga gari mojawapo na kusababisha kugongana yenyewe kwa yenyewe,” alisema Kamanda Mkondya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles