Christina Gauluhanga, Dar es Salaam
Tume ya Ushindani (FCC), imefanya ukaguzi katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2017/2018 wa makontena 3,312 na kubaini kontena 142 zilikuwa na bidhaa bandia.
Akizungumza na Mtanzania Digital leo Julai 5, katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkurugenzi wa Utekelezaji Sheria, Dk. John Nangala amesema ukaguzi huo ulifanywa mikoa mbalimbali na mipaka yote ya nchi.
“Katika kipindi hiki pia tulifanya kaguzi za kushtukiza 31 katika maeneo mbalimbali nchini, na tumefanya ukaguzi katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Mwanza, Arusha, Mbeya na mipakani,” amesema.
idha Nangala amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kujenga uelewa wa bidhaa bandia na katika kipindi hicho wamepokea kesi za ushindani malalamiko 60.