24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KONGOLE SHERIA KALI KWA MALORI YANAYOZIDISHA UZITO

Na JUSTIN DAMIAN


UJENZI wa barabara kwa kiwango cha lami ni moja kati ya hatua kubwa za kimaendeleo ambayo Tanzania inaweza kujivunia.

Kama ilivyo kwa nchi nyingine zinazoendelea, Tanzania  ina matatizo na vipaumbele vingi lakini katika miaka 15 iliyopita, nguvu kubwa imeelekezwa kwenye ujenzi wa barabara.

Kutokana na ujenzi wa barabara, kwa sasa mikoa karibu yote imeunganishwa  kwa barabara za lami, hivyo kufanya usafirishaji wa mizigo pamoja na watu kuwa rahisi, jambo ambalo linachangia maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Miundombinu mizuri ya barabara imekuwa si ya faida tu kwa Tanzania, bali hata nchi jirani ambazo hazina bandari kama Burundi, Rwanda, Uganda, Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hata hivyo, pamoja na kuwa na matumizi ya barabara kusafirisha mizigo kwenda nchi jirani, yameleta neema kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na ushuru unaotokana na matumizi ya bandari ambayo hupitisha mizigo ya nchi jirani. Changamoto ya uharibifu wa barabara nayo imeibuka kutokana na malori kuzidisha mizigo zaidi ya kiwango kilichopangwa.

Ujenzi wa barabara unagharimu fedha nyingi. Ujenzi wa kilomita moja kwa kiwango cha lami unakadiriwa kufikia  zaidi ya Sh bilioni moja. Pamoja na kwamba barabara zinajengwa katika ubora, zimekuwa hazidumu muda mrefu kutokana na uharibifu unaofanywa na malori yanayozidisha mizigo.

Ni jambo la kusikitisha kuona fedha za walipakodi masikini wa Kitanzania zinazojenga barabara zikihujumiwa na wasafirishaji mizigo kutoka nchi jirani. Hata hivyo, baada ya kipindi kirefu cha uharibifu, sasa tatizo hili huenda likapata mwarobaini kutokana na  Sheria ya Kudhibiti Mizigo kwa Magari ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2016 ambayo utekelezaji wake utaanza Januari mosi mwakani.

Kupitia sheria hiyo, faini kutokana na kuzidishi uzito itaongezeka kutoka Dola za Marekani 2,000 (Zaidi Sh milioni 4 hadi kufikia Dola za Marekani 15,000 (Zaidi ya shilingi milioni 30) atakapokamatwa mkosefu.

Hatua ya utekelezaji wa sheria hii ni ya pongezi kwa kuwa sasa waliokuwa wanazidisha mizigo watakuwa macho kutokana na uwepo wa adhabu kali.

Cha msingi ni kuwa watu watii sheria bila ya shuruti na hivyo kutopatikana na adha ya faini kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles