26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kongamano kuwafunda vijana kiuchumi laja

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wanafunzi wa vyuo, waendesha bodaboda na makundi mengine ya vijana wanatarajia kupatiwa mafunzo yanayolenga kutambua mchango wao katika kujenga uchumi wa taifa.

Kongamano hilo litakalofanyika Dar es Salaam wakati wa Siku ya Vijana Duniani inayoadhimishwa Agosti 12 kila mwaka limeandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na uwezeshaji vijana, wanawake, watoto na watu wenye uhitaji maalumu.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 19,2023 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Amina Said, amesema wanatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ndiyo maana wameweka mikakati ya kuwezesha kundi hilo kwa lengo la kutatua changamoto za ajira zinazolikabili.

“Amo inalenga kumuamsha kijana kujitambua na kujua thamani yake, kijana asipojielewa na kujithamini hata ufanye vipi ni kazi bure.

“Amo inamuamsha kijana aweze kujiongoza mwenyewe na kutimiza malengo yake binafsi,” amesema Amina.

Amesema pia katika kongamano hilo vijana watapata nafasi ya kujifunza mambo mbalimbali kama kujitambua, biashara na uwekezaji, masoko, umuhimu wa kutii sheria na fursa zinazopatikana nchini na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kujisajili.

Mkurugenzi huyo amesema watawawezesha vijana kwa kuwapatia vitendea kazi kama vile bodaboda, vyerehani, mitungi ya gesi na majiko yake.

Naye Mwalimu wa Saikolojia katika shirika hilo, Neema Bachu, amesema wataanza Dar es Salaam kisha kwenda katika mikoa mbalimbali kwa sababu tayari wamepokea maombi ya kuwafikia vijana.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo lenye kaulimbiu isemayo ‘Uwajibikaji wetu ndio uhai wa uchumi wetu’ anatarajiwa kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles